Unasoma ILI IWEJE?


Nafurahi kuwa Jf na member kama wewe!
Kuna linalo weza kufanyika kufanya elimu yetu more practical?
Cc mpigamsuli
 
Last edited by a moderator:
Nafurahi kuwa Jf na member kama wewe!
Kuna linalo weza kufanyika kufanya elimu yetu more practical?
Cc mpigamsuli

Tungeacha vile vitu ambavyo hatuna uwezo navyo kwa hao waliovianzisha au wenye uwezo navyo. Sisi elimu yetu ikajikita kwenye kilimo na ufugaji, ikiwezekana na mambo ya ujasiriamali. Hapo hata tusingekua na mjadala wa tutumie kiswahili au kiingereza kufundishia, tungetumia kiswahili tu kwa sababu kila kitu kipo wazi.

Mambo ya electronic, sijui nyuklia tuwaachie haohao, tukihitaji hizo huduma tuta nunua kutoka kwao. Nilishawahi kusema na leo narudia tena, tuna akili sana sema tu hatujajua namna ya kuziwekeza kwenye maeneo stahiki tukafaidi matunda yake. Elimu yetu ni ya kinadharia na kufikirika sana. Mwalimu anamfundisha mtoto atom au cell kitu ambacho kimsingi hata ule mfano wa hicho kitu halisia hajawahi kukiona. Mara unamfundisha mapigo manne ya injini, umewahi kujiuliza ni nini kinakua kinaendelea kwenye vichwa vya wanafunzi wakati wa hizo topic? Kisha unategemea upate wataalam wanaoelewa vizuri.

Tukubali kubaki na mambo machache tukayafanya vizuri na kuelekeza nguvu kazi zetu huko, nna imani matunda yataonekana.
Tukiwa na wahitimu wa darasa la saba weney uelewa mzuri juu ya kilimo naufugaji, hali kadhalika wahitimu wa kidato cha nne na sita hadi vyuo, tutakuwa na vijana wanaotamani kuona wanaitumia elimu yao kwa vitendo zaidi ukizingatia ardhi tunayo ya kutosha. sitategemea nchi yetu kuendelea kuombaomba misaada ya chakula wakati tuna kila kitu.
 
Nasoma nije niwe mbunge au waziri hivyo ndivyo watoto wa siku hizi husemaga
 
nasoma ili nije kuajiri wasomi waniendelezee biashara yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…