Unatafuta ushahidi wa mapenzi ya Wazanzibari kwa Maalim?

Mwalim wetu Sheikh Mohamed Said ,,.
Tafadhali Hebu tupe kisa hiki kwa urefu tupate elim mpya Juu ya rais huyu Abood jumbe mwinyi ikawaje mpk akatolewa na kuwekwa kigamboni..

Ikikupendeza Hata kwa ishara utupe aloitoa hyo barua na Mzee Jumbe krj Maelezo yake amesemaje nn lilikuwa wazo lao ktk Muungano..

Shukran
 
Always...
Ingia humu ndani:
http://mohamedsaidsalum.blogsp...umbe-mwinyi-1920-2016.html?m=1
 
jazia nyama mzee...japo nimekuelewa ila bado umeniacha na kiu...ya kutaka kumfahamu MAREHE Maalim Seif
 
Na hapo bado kuna tulioshindwa kwenda kwa sababu tofauti tofauti. Kwa Hakika Maalim alikuwa the Lion King


Allah Ampumzishe pumziko lililo jema Jemadari wetu. Kipenzi chetu... Ameen
 
Kuna tetesi zinasema kwamba Maalim alimchoma Marehemu Abdul Jumbe alipotaka kuitoa Zanzibar toka kwenye Muungano, ndio ikapelekea Jumbe kutolewa uanachama na urais wa Zanzibar.

Hizo ni moja ya porojo za wana CCM katika kujaribu kumchafua Maalim Seif, siku zote Binaadamu wakishaishiwa kwa hoja huishia na propaganga za kipuuzi kabisa
 
Hizo ni moja ya porojo za wana CCM katika kujaribu kumchafua Maalim Seif, siku zote Binaadamu wakishaishiwa kwa hoja huishia na propaganga za kipuuzi kabisa
Dos...
Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nikaelezwa kuwa serikali ya Tanzania iliamua kumfukuza Mufti Sheikh Hassan bin Ameir Tanganyika kwa sababu alikuwa anapanga njama za kupindua serikali.

Hii ilikuwa 1968.

Mwaka wa 1964 babu yangu akiwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Association (TRAU) alikamatwa na kuwekwa kizuizini na sababu alizoelezwa baba yangu na rafiki zake ndani ya serikali ni kuwa yeye na viongozi wenzake katika vyama vya wafanyakazi walikuwa wanapanga njama za kupindua serikali na kumuua Rais wa nchi.

Mambo ya kutisha.
Propaganda za kipuuzi kama ulivyosema.

Nasoma kitabu cha maisha ya Julius Nyerere kilichoandikwa na Prof. Issa Shivji na wenzake nakuta imeandikwa kuwa EAMWS imemunjwa kwa kuwa ilikuwa inaongozwa na ''tycoons'' Wahindi.

Hii ndiyo sababu iliyoelezwa.

Lakini kilichonisikitisha sana ni kule kuandikwa kuwa EAMWS imevunjwa wakati inajenga Islamic Centre.

Wamepata hofu kusema kweli kuwa EAMWS ilikuwa inajenga Muslim University kwani wakisema hivyo hiyo hoja ya kuwa ilivunjwa kwa sababu ilikuwa inaongozwa na matajiri Wahindi itaporomoka.

Wanauogopa ukweli kusema kuwa EAMWS imevunjwa ili kuwakosesha Waislam Chuo Kikuu na hivyo elimu.

Huyo ''tycoon'' katika EAMWS alikuwa Aziz Khaki.
Mtanzania wa kawaida katika jamii ya Ismailia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…