Unataka kuanza ujenzi? Hii option nafuu zaidi

Sijaelewa.

Hesabu za kwanza umeonyesha jumla ni 7M tuassume ni 8M na za pili umeonyesha 2M tuassume ni 3M. Ambayo jumla yake inakua 11M.

Kisha umesema ukijumlisha finishing inakua 35M mpaka 40M.

Nini kinafanya hesabu zilizosound simple kufikia 40M?
 
Hv kwa sasa n style ipi kali ya kujenga nyumba kat ya nyumba za kawaida na za contemporary? Raman kali unauzaje? Nkiwa na milion 35 serious nahamia kwangu!!
 
Nyumba ndoto yangu;Naishi nayo kwenye ndoto!
 
Finishing,
Finishing ndio itaifikisha gharama huko,
ukicheki material yaliyoolodheshwa nyumba haikamiliki kuwa hivo inavoonekana.
Hapo bado kuna ishu za Plaster, tiles, rangi, milango, madirisha, mifumo ya maji na umeme n.k
 
Hv kwa sasa n style ipi kali ya kujenga nyumba kat ya nyumba za kawaida na za contemporary? Raman kali unauzaje? Nkiwa na milion 35 serious nahamia kwangu!!
Tunatofautiana boss,
Interest yako ndio itaamua ‘ipi ni style kali’, japo hizo contemporary ni kisasa zaidi.
Yes kwa hesabu ya hiyo itacheza kwenye range hiyo ya gharama kama kiwanja hakitokua na changamoto. Na kuna baadhi ya maeneo inaweza hata kupungua.

Ila Naona kuna comments raia wengine wanaona kama 35Ml ni nyingi kwa nyumba iliyokamilika😁.
 
Nyumba hii inakua wazi upande wa nyuma, hivi hakuna gutter.

hii unamaanisha nini?
Kwa kawaida nyumba za mtindo huo huwa na mitaro (gutters) ya kupokea maji kutoka kwenye bati, amabyo hujengwa kwa zege la nondo na then waterproofing materials. Hiyo maji mwagika nyuma tu kunakuwa wazi.
Kuna post nilielezea hilo na niliweka picha
 
Hapo kwenye 35-40 ndio umeharibu...kwaheri
Huo ndio uhalisia, nimeweka idadi ya material na gharama zake ili mtu apate picha kamili.

Sasa ukiangalia hapo Finishing ndio itaifikisha gharama huko,
ukicheki material yaliyoolodheshwa nyumba haikamiliki kuwa hivo inavoonekana.
Hapo bado kuna ishu za Plaster, tiles, rangi, milango, madirisha, ceiling, mifumo ya maji na umeme n.k
Yani ulitegemea nyumba ya vyumba vitatu, dining, sebule, jiko, store na choo
Ikamilike na kila kitu kwa Ths 10Ml.
Wabongo tunapenda vitu rahisi ndio maana matapeli wengi na wapya kila siku.
 
Finnishing ndo kifo cha pesa kwenye ujenzi wa nyumba.
 
Kupau 2mil? Mimi fundi tu nilimpa 1.5...kupaua ilicost almost 11 mil
Ninauhakika na nilichokiandika boss.
Angalia idadi ya material, angalia aina ya design, ukubwa wa jengo, na labda kama haujaelewa basi uliza, usikalili. Hapo gharama ya ufundi/kupaua haijaandikwa lakini kwa design hiyo ufundi haizidi 1ml
 
Hizo bati zina upana gani na urefu gani? Ndugu mtaalam.
 
Usikariri.

Sio usikalili.

Una matatizo ya kuandika. Utaalam huu wa ujenzi ilijifunza vyuoni au kwa mazoea ya kusindikiza na kubeba vyombo vya mafundi wakubwa?
Umeanza Mkuu na vurugu zako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…