Unataka kumuacha mke mkorofi? Fanya hivi

Unataka kumuacha mke mkorofi? Fanya hivi

Mgombezi acha ujinga wewe, Nani kakwambia kua ni lazima ukipata mwingine atakua na matatizo zaidi? Hizo ni imani mbovu zinazowafanya wanandoa wasiwe na amani kakti maisha yao, wawe watumwa wa wenzao, na kufanya mapenzi nje ya ndoa zao. Uvumilivu unakikomo bwana, baada ya hapo hakuna mapenzi tena...ni mateso tuu!
Nimepigia mstari tu kaka......................
 
Mgombezi acha ujinga wewe, Nani kakwambia kua ni lazima ukipata mwingine atakua na matatizo zaidi? Hizo ni imani mbovu zinazowafanya wanandoa wasiwe na amani kakti maisha yao, wawe watumwa wa wenzao, na kufanya mapenzi nje ya ndoa zao. Uvumilivu unakikomo bwana, baada ya hapo hakuna mapenzi tena...ni mateso tuu!

Mkuu LexAid; Tena naongezea kusema usije ukaruka mkojo na ukajikuta unakanyaga mavi. Watu wanaotafuta the right person, wao ndiyo wenye matatizo.
 
Du! naona umeingia na kutoka! haujataka kuzama indeep katika njia ya kummwaga mke mkorofi, mpenzi mkorofi is very easy, but not for wife..! I'm still waiting....! kuona ni njia ipi mbadala ya kuitumia kwa mke/mme mkorofi.
 
Uvumilivu unakikomo bwana, baada ya hapo hakuna mapenzi tena...ni mateso tuu! Nimepigia mstari tu kaka......................

UVUMILIVU haupaswi kuwa na kikomo; utashindwa kuvumilia. Matatizo ya wanadamu yanatofautiana; vilevile kumbuka UVUMILIVU unapaswa kuendana na KUCHUKULIANA. Yaani unamwelewa mwenzako katika udhaifu wake.
 
Mgombezi acha ujinga wewe, Nani kakwambia kua ni lazima ukipata mwingine atakua na matatizo zaidi? Hizo ni imani mbovu zinazowafanya wanandoa wasiwe na amani kakti maisha yao, wawe watumwa wa wenzao, na kufanya mapenzi nje ya ndoa zao. Uvumilivu unakikomo bwana, baada ya hapo hakuna mapenzi tena...ni mateso tuu!
Kuna mtu mwingine anajijua lakini hataki kujirekebisha lakini wakimwagana kwa mpya atakaekuja anaweza akajirekebisha! matatizo yake.
 
Heshima yako baba,
Naamini kila ndoa haikosi mojawapo ktk hayo,
Na sio yote yanafanywa na wanawake tu kuna mengine unamkuta mwanaume ndio kbs,
Kilichopo ni kuomba mungu na kupata hekima ya kuishi na mwenza wako,
All in all tasisi ya ngoa ni pasua kichwa tu sema watu wanavumiliana tu.
 
UVUMILIVU haupaswi kuwa na kikomo; utashindwa kuvumilia. Matatizo ya wanadamu yanatofautiana; vilevile kumbuka UVUMILIVU unapaswa kuendana na KUCHUKULIANA. Yaani unamwelewa mwenzako katika udhaifu wake.
Ni kweli mkuu, hata kama anakuua wewe vumilia tu, ile uende mbinguni...........................LOL
 
Thank God kwa sasa mada hii hainihusu!

But some years ago... Man..! I almost plotted a murder..!

Na nadhani it will take time for me to find another wife...
 
Ni kweli mkuu, hata kama anakuua wewe vumilia tu, ile uende mbinguni...........................LOL
Du! mkuu hapa nimecheka ndio maana nilisubiri majibu!
UVUMILIVU wa tabia na matendo mmh hapo ndipo panakapokuwa pagumu.

Kama mtu kakutilia sumu ukapona maana kakukosakosa, sasa mtu kama huyo siku akikupatia timing umekwenda na maji, kama aliweka nusu kijiko! ataweka vijiko vitatu kabisa!
 
Kwa usemi huu mchakato wa kuhakikisha mama anarudi b4 weekend unaanza rasmi. Ila kesho nitaugua ili usiende job (ni valentine, tunamsaidia maza kukuchunga)
Samahani dingi, natamani advice ingejumuisha na kinamama manake hata wamama wanaopitia mateso haya ni wengoi pia.
Mimi kwa mama CantaNgina nimefika.............Nawashauri wenye ndoa pasua kichwa...........
 
Da' AshaDii, mie mzima wa Afya, hofu na mashaka ni kwako wewe na familia yako mlioko mbali na upeo wa macho yangu, na utakapo kujua khali zetu, mie na familia yangu tuwazima wa afya na tu salama buheri....................
Asalaaamu Aleikhum Da AshaDii...............

Baada ya salaam, ningependa tu kusema kuwa naheshimu sana maoni yako, na huwa nafarijika saana pale nionapo neno lako kwenye uzi wowote ninaoutundika humu.

Pamoja Daima................

Mtambuzi salamu zako zimenifurahisha kweli kweli.... Ni wazi umefurahi kuniona.... Asante Dear... Mimi ni mzima wa afya pamoja na familia yangu yoote, namshukuru Mungu. Na nafurahi kua pande zako ni nzuri pia.

I am always humbled by your appreciation ya michango yangu, na mimi pia huguswa/furahiswna na chekeshwa/hamasishwa na pia hujifunza toka katika mambandiko yako, hua mara nyingi wanipa a man's perspective kwa vitu vya msingi na in a serious note. Napenda saana understanding the opposite sex... na mara nyingi hua wanipa hio...

Pamoja Saana.
 
Nadhani wasingewaoa toka awali. Kweli mkorofi wa hivyo anafichaje makucha hadi anaolewa? Au wakati wa kumuoa macho yalikuwa kengeza kila kitu yaliona sawa tu, kishaolewa na kuzaa watoto then talaka zije?? Nashauri wasiwaoe kabisa watu kama hao.
 
Maana mimi nachukia kuachana asema BWANA Mungu wa Israel ... awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana malaki 2: 15.

Mimi nilichemsha kabisa...

Ndoa kanisani,MC maarufu kabisa Dar... Bebana beach ya Aga khan na picha kibaaaoo... Mapumziko Sheraton (enzi hizo)kwa siku moja,na ile hoteli ya Mnyakyusa pale opp na River Side ndiyo honey moon...

Still nilimchoka baada ya 4 years,na hapo ni baada ya kuvumilia muda mrefu matatizo yake... She was never a cheater... Huenda alikuwa anacheat,sijui... Ila kero zake ni kama hapo juu...

Baada ya kupart naye,weight yangu imeongezeka abruptly...! Na kila mmoja anashangaa!
 
Kwa usemi huu mchakato wa kuhakikisha mama anarudi b4 weekend unaanza rasmi. Ila kesho nitaugua ili usiende job (ni valentine, tunamsaidia maza kukuchunga)
Samahani dingi, natamani advice ingejumuisha na kinamama manake hata wamama wanaopitia mateso haya ni wengoi pia.
Waweza fungua hizi Link hapa chini:
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/170442-namna-ya-kumpiga-kibuti-mume-mkorofi.html
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/170590-kumpiga-kibuti-mume-mkorofi-muendelezo%85%85.html
 
Nadhani wasingewaoa toka awali. Kweli mkorofi wa hivyo anafichaje makucha hadi anaolewa? Au wakati wa kumuoa macho yalikuwa kengeza kila kitu yaliona sawa tu, kishaolewa na kuzaa watoto then talaka zije?? Nashauri wasiwaoe kabisa watu kama hao.

Mpendwa Digna37, si mara zote wakati "tunapenda" tunakuwa macho wazi kuona kila jema na baya la mwenzetu. Tukumbuke kuwa kipindi cha uchumba ni kipindi cha "kujiuza" mbele ya mwenzako kwa hivyo wengi hufanya kila hali kuonesha yale yaliyo mazuri tu, tena kwa nia safi kabisa, na pengine mhusika hukusudia aendelee kuwa vile vile alivyotaka aonekane. Lakini kujirekebisha tabia mbaya ndani ya mwendo ni shida, na ndio hapo hujitokeza wenyewe wakati ukifika.

Vilevile Mtambuzi aligusia hapo juu jinsi watu wanavyobadilika baada ya muda, kutokana na kiburi, kipato, kujiamini kupita kasi na kadhalika. Na hilo si kwa wanawake tu, na wanaume pia. Sasa inapofikia mtu kabadilika 180º na umejaribu kusaidiana naye kurekebisha hali hiyo lakini imeshindikana, njia nzuri kwa usalama wako na wake ni kukata mzizi wa fitina, ili mjipe fursa na wakati wa kuishi kwa amani.

Kitu ambacho ningependa kuwashauri wanandoa, wawe makini kuyaangalia haya mambo mapema na sio kuendelea kuvumilia miaka yote hiyo wakijua kuwa uwezekano wa kupatikana nafuu ni mdogo. Si vibaya kuanza upya, lakini unang'ang'ania tu huku miaka inapita, pengine na watoto na majukumu yanaongezeka...mpaka inafikia hadi unahisi bora uendelee kuteseka tu. Maamuzi magumu na muhimu bora kuyachukua mapema.

Naungana na Mtambuzi, talaka isiwe kimbilio la kwanza. Talaka iwe hatua ya mwisho kabisa baada ya kuwa umemaliza "karata zote". Na pale inapobidi, kata kamba, mbele kwa mbele.
 
Heshima yako baba,
Naamini kila ndoa haikosi mojawapo ktk hayo,
Na sio yote yanafanywa na wanawake tu kuna mengine unamkuta mwanaume ndio kbs,
Kilichopo ni kuomba mungu na kupata hekima ya kuishi na mwenza wako,
All in all tasisi ya ngoa ni pasua kichwa tu sema watu wanavumiliana tu.
Kuna yule jamaa wa Arusha alifika bei, hebu niambie mlimalizana vipi ili nijue kama nachukua changu mapema, maana siku hizi sioni hata ukifanya bidii na masomo, Ibilisi keshakuingia wewe.....................
 
Back
Top Bottom