Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 878
- 2,014
Nipo zangu kwenye mgahawa, napata menu, halafu kuna binti naye yupo hapa. YAAANI mwanamke msumbufu kwenye kuagiza chakula mpaka unaanza kujiuliza huyo jamaa wake huko nyumbani anapitia nini.
Akaletewa wali na nyama. Lakini haikuchukua sekunde nyingi, akaanza malalamiko—nyama ina mafuta. Mhudumu, kwa ustaarabu wake, akambadilishia. Baada ya kula vijiko viwili, akaita mhudumu tena: "Samahani, naomba chumvi, lakini pia huu wali una kiini." Ikumbukwe, sisi wengine tunakula wali huo huo na upo sawa tu.
Bado mambo hayajaisha. Akaagiza soda. Soda imefuka kidogo, akalalamika: "Hii haina ule unaridi nilioutegemea." Wahudumu wakamweleza kwa upole kuwa cha baridi sana ni juisi ya matunda, maana imekaa muda mrefu kwenye friji. Badala ya kuelewa, akaanza kubwabwaja juu ya hatari ya kuumwa tumbo kwa kunywa juisi hiyo. Ikumbukwe, sisi wengine tunakunywa juisi hiyo hiyo na hakuna anayelia.
Kwa nilichoshuhudia hapa, nimepata litmus test matata kwa wanaopanga kujivutia jiko ndani. Unataka kujua huyo mwanamke kama mtawezana? Mpeleke kwa Mama Ntilie. Kama ataita muhudumu mara tatu kwa mambo madogomadogo ambayo yanaweza kuvumilika, tambua kuwa huko mbele kuna safari ngumu. Lakini kama anaweza kula kilichopo bila visingizio vya kila dakika, basi pengine huyo anaweza kuwa chaguo sahihi.
Maisha siyo Instagram. Uvumilivu kwa mambo madogo huakisi uwezo wa kuvumilia changamoto kubwa. Kama mwanamke anaweza kufanya wahudumu wakakimbizana kwa amri zake zisizoisha kwa mlo mmoja, vipi itakavyokuwa kwenye ndoa? Kaka, zingatia.