Unataka pesa? Ingia kwenye kilimo cha maboga

Unataka pesa? Ingia kwenye kilimo cha maboga

Motivational speaker wamechafua hali ya hewa hadi watu wamezidisha tahadhari. [emoji38]

Jamani, bado wapo watu wenye wazo au jambo la manufaa la ku-share nasi kama huyu. Tuwape nafasi ili tunufaike na ujuzi badala ya kuhofia kila mada ni Motivational speaker
 
Tupe basi zile hesabu [emoji23][emoji23][emoji23]
Eka moja hutoa maboga 10000 ambapo kila boga utauza 4000 ikiwa soko baya 2000
Ukipiga na kutoa gharama za uendeshaji[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] malizia bro

Kila kitu unawekeza 2m na masoko ya kumwaga yaani chap chap unapata 4m faida ila ukisubiri unaweza pata hata 5.5m
Ingia sasa
 
Boga ni zao ambalo mmea wake unakuwa kwa kutambaa na ni la mviringo, ngozi yake ni nyororo na rangi yake ni ya njano inayoelekea kwenye rangi ya chungwa au rangi ya kijani. Katikati ya boga kuna mbegu na massa, Boga lipo katika jamii ya Cucurbita pepo.

Asili yake
Asili ya boga ni Amerika kaskazini, maboga yamekuwa yakipandwa kwaajili ya biashara na kwaajili ya chakula. Kwa sasa maboga yamekuwa yakilimwa maeneo mbalimbali duniani, Antarctika pekee ndiko maboga hayawezi kustawi. Mataifa yanayozalisha maboga kwa wingi ni Marekani (USA), Canada, Mexico, India, and China.

Hali ya hewa & udongo
Maboga yanahitaji joto la wastani kutoka kwenye jua, pia eneo ambalo halituamishi maji udongo wake uwe na pH kati ya 6.0 – 6.8. Pia udongo uwe na joto inchi tatu (sm 7.6) kushuka chini angalau nyuzi 60 °F (15.5 °C), maboga yatadhoofika kama maji yatakosekana.

Utayarishaji wa shamba
Shamba litayalishwe kwa umakini bila kuwa na sehemu ya kutuamisha maji maana mmea wa maboga na maboga yenyewe hutambaa chini, tumia jembe la ng’ombe, trekta, jembe la mkono au pawatila, changanyia mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha shamba.

Utayarishaji wa mbegu
Mbegu za maboga zinatoka ndani ya maboga, kuna mbegu zilizoboreshwa (za kisasa) na za asili, andaa mbegu mapema wiki moja au mbili kabla ya kupanda.

Upandaji
Maboga hupandwa kwa kufukia mbegu sentimita 1 au 2 chini ya udongo , panda mbegu 2 kila shimo. Pia panda umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 2 kutoka mstari hadi mstari.

Matandazo (mulches)
Kwasababu ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika ardhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.

Mbolea
Katika matumizi ya mbolea yanatofautiana kutokana na mbegu, Lakini tumia mbolea za asili (samadi au mboji) ili kuongeza rutuba kwenye udongo, ukihitaji kutumia mbolea za viwandani weka kiasi sana, labda eneo hilo kama hakuna rutuba, mbolea ya NPK inaweza tumia.

Upaliliaji & unyevu
Palilia shamba nyasi zinapoanza kuota, pia safisha shamba ili kuondoa wadudu. Shamba la maboga linatakiwa liwe na unyevunyevu kila mara ili maboga yaweze kustawi vizuri yasidumae.

Uvunaji
Maboga hukomaa baada ya siku 95 mpaka 120, ili kujua kuwa boga lako limekomaa unaangalia kikonyo, kikonyo cha boga kinapoteza maji na kinaanza kuwa kikavu.

View attachment 2088484
𝐍𝐢𝐦𝐞𝐢𝐩𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐡𝐢𝐢𝐢
 
Ilianza pilipili, mayai ya kware, ufugaji wa sungura, kilimo cha tikiti maji, vitunguu saumu, kwa sasa maboga,
Kuna mmpja namfahamu alipigwa kwemye tangawizi japo tulimuonya.
Jamaa kampuni hewa walisuka mpango wa kuwauzia mbegu za tangawizi watu wajinga.
Wakamwambia kuwa akivuna tangawizi atapata milioni 54 kwa heka, mbegu wanakuuzia wenyewe sh. Laki 8 kwa gunia.
Jamaa akanunua mbegu akalima robo heka.
Kilichomkuta anajua mwenyewe, yani jamaa wa kampuni wlipotea hewni na tangawizi zake akauza 1500 / kilo kwenye masoko ya kawaida.
 
Fursa ya maboga ni kwenue mbegu tu, nasikia wajindi waliingia kyela huko kununya mbegu za maboga wanaenda kikamua mafuta na kupata mashudu kwa ajoli ya wnyama.
Tufanye urafiti ni maboga gani yanatoa mbegu za kutosha oli wakilima wayalome kwa wi gi tupate mafita mashudu na unga waaboga kwa ajili kuchanganya kwenye unga wa lishe na .
TULIME maboga wakuu, fursa ipo ila imejilalia usingizi, iwapi mtu atakuwa smart MABOGA! yatamtoa.
Nampango wa kulima kama heka 5 na heka 6 za vuazi lishe nione itakuwaje.
Ntalima kilomo mseto, shinyanga tulikuwa tunalima manoga ndani ya shamba la mahindi na yanazaa sana, hakuna gharama kulima maboga wakuu.
 
Tupe basi zile hesabu [emoji23][emoji23][emoji23]
Eka moja hutoa maboga 10000 ambapo kila boga utauza 4000 ikiwa soko baya 2000
Ukipiga na kutoa gharama za uendeshaji[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] malizia bro
Hizi hesabu zinakuwaga hatari sana😂😂😂
 
Piga hesabu za mbali
Mbegu huko mnatupa huku watu wanakula
Chini ya 200gm Sh 6000
Hapa tunaita entrepreneur siyo Mkulima tena
IMG_4332.jpg
 
Umemaliza ama bado unaendelea? Fafanua zaid faida zake kiuchumi maana wengi tunajua linatumika kama chakula tu na majani yake hutumika kama mboga. Je, kuna matumizi mengne ya ziada?
Ni chakula kizuri cha mifugo hasa [emoji200]
 
uzi ungekuwa wa tofauti km ungekuja na mbegu yenye uwezo wa kuzalisha maboga yenye mbegu nyingi zaidi. kilo ya mbegu za maboga local market 8000. watafiti kujeni mlete breed nzuri ya kuzalisha mbegu nyingi
 
Back
Top Bottom