Unatakiwa ufanye hivi, unapokutana na simba uso kwa uso

Unatakiwa ufanye hivi, unapokutana na simba uso kwa uso

Daah sidhani kama utaweza kukumbuka cha kufanya unapokutana na Simba navyomuona yeye anatuona kama sisimizi tu akiamua anakuacha au anakujeruhi ila sio kwamba pana kitu unaweza kufanya na mikono yako ukapambana nae au sijui mnadanganyana eti ukimuangalia ana aibu..
 
Attachments

  • 20231209_154537.jpg
    20231209_154537.jpg
    1.6 MB · Views: 4
  • 20231209_155304.jpg
    20231209_155304.jpg
    1.7 MB · Views: 1
  • 20231209_163033.jpg
    20231209_163033.jpg
    468.5 KB · Views: 3
  • 20231209_165719.jpg
    20231209_165719.jpg
    623.2 KB · Views: 4
Daah sidhani kama utaweza kukumbuka cha kufanya unapokutana na Simba navyomuona yeye anatuona kama sisimizi tu akiamua anakuacha au anakujeruhi ila sio kwamba pana kitu unaweza kufanya na mikono yako ukapambana nae au sijui mnadanganyana eti ukimuangalia ana aibu..
Jamaa mmoja anaitwa Samson, nasikia alipambana na simba na kufanikiwa kumrarua. Kwahiyo inawezekana tu ukijiamini
 
Si lazima awe simba, maisha.. maisha yaache kama yalivyo ndugu. Sekunde moja tu inatosha kabisa kubadilisha maisha na hatma ya mtu. Tunaangalia sana filam, makala hasa zile zinazo elezea matukio halisi yaliyo watokea watu, hapo utagundua kuwa hatma yetu ni fumbo zito.
 
Jamaa mmoja anaitwa Samson, nasikia alipambana na simba na kufanikiwa kumrarua. Kwahiyo inawezekana tu ukijiamini
Mbwa tuu anakua ndio uje kwa Simba nimetuma picha hapo maana mnaweza kudhani ni Simba wa kuchora..
 
Mh, tuombee isitokee, lakini kama imetokea na umekutana naye ili asikudhuru unatakiwa ufanye kitu hiki ni kigumu lakini unatakiwa ukifanye:

Simama mwangalie macho kwa macho huku ukiondoa hofu!!! Simba humuogopa binaadamu hivyo atakupa hiyo heshima endapo usipomuonyesha hofu!!!!! Utaweza????

View attachment 2883494

Experts say the key to a thrilling lion encounter is respect. Keep your distance and understand — but don't blindly fear — the lethal capabilities of Africa's most fascinating cat. Humans are actually much more dangerous to lions than they are to us.

Simba yule mbwa koko wa jirani yako au simba simba wa Masai Mara na Tsavo?
 
Kuna mjinga mwingine aliniambia eti ukishikwa na Mamba Ziwani/Mtoni kitu cha kukuokoa unatakiwa kumbinya machoni anakuachia haraka sana, sasa unajiuliza hapo una wenge la kukamatwa na dude kama lile halafu hapohapo una wenge la kurushiwa majini utapata hilo wazo la kumbonyeza jichoni kweli
 
Huu ni mtego na kamwe sitauingia (Kwa Sauti ya Kabudi Palamaghamba)

😃
 
Ukutane na simba umuangalie usoni alafu uondoe hofu!!

Ni rahisi eeeenh??? Vitu vingine mnaongea tu
Inawezekana mkuu hasa ukiwa unatambua kwamba hiyo ndio njia pekee ya kukuokoa.
 
Kwanini Simba huitwa Mfalme wa pori?
Simba awapo na njaa Kila kilicho mbele yake ni harali yake, haijalishi ataua au atakufa.
 
Back
Top Bottom