Unatakiwa ufanye hivi, unapokutana na simba uso kwa uso

Daah sidhani kama utaweza kukumbuka cha kufanya unapokutana na Simba navyomuona yeye anatuona kama sisimizi tu akiamua anakuacha au anakujeruhi ila sio kwamba pana kitu unaweza kufanya na mikono yako ukapambana nae au sijui mnadanganyana eti ukimuangalia ana aibu..
 

Attachments

  • 20231209_154537.jpg
    1.6 MB · Views: 4
  • 20231209_155304.jpg
    1.7 MB · Views: 1
  • 20231209_163033.jpg
    468.5 KB · Views: 3
  • 20231209_165719.jpg
    623.2 KB · Views: 4
Jamaa mmoja anaitwa Samson, nasikia alipambana na simba na kufanikiwa kumrarua. Kwahiyo inawezekana tu ukijiamini
 
Si lazima awe simba, maisha.. maisha yaache kama yalivyo ndugu. Sekunde moja tu inatosha kabisa kubadilisha maisha na hatma ya mtu. Tunaangalia sana filam, makala hasa zile zinazo elezea matukio halisi yaliyo watokea watu, hapo utagundua kuwa hatma yetu ni fumbo zito.
 
Jamaa mmoja anaitwa Samson, nasikia alipambana na simba na kufanikiwa kumrarua. Kwahiyo inawezekana tu ukijiamini
Mbwa tuu anakua ndio uje kwa Simba nimetuma picha hapo maana mnaweza kudhani ni Simba wa kuchora..
 
Simba yule mbwa koko wa jirani yako au simba simba wa Masai Mara na Tsavo?
 
Kuna mjinga mwingine aliniambia eti ukishikwa na Mamba Ziwani/Mtoni kitu cha kukuokoa unatakiwa kumbinya machoni anakuachia haraka sana, sasa unajiuliza hapo una wenge la kukamatwa na dude kama lile halafu hapohapo una wenge la kurushiwa majini utapata hilo wazo la kumbonyeza jichoni kweli
 
Huu ni mtego na kamwe sitauingia (Kwa Sauti ya Kabudi Palamaghamba)

😃
 
Ukutane na simba umuangalie usoni alafu uondoe hofu!!

Ni rahisi eeeenh??? Vitu vingine mnaongea tu
Inawezekana mkuu hasa ukiwa unatambua kwamba hiyo ndio njia pekee ya kukuokoa.
 
Kwanini Simba huitwa Mfalme wa pori?
Simba awapo na njaa Kila kilicho mbele yake ni harali yake, haijalishi ataua au atakufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…