Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wengi wanatamani kumiliki biashara kubwa kubwa, lakini mwisho wa siku wanakuwa ni watu wa kutamani tu, wakianzisha biashara kesho watafunga na wataamia nyingine na mwisho wa siku hakuna biashara tena. Ni vizuri kufahamu makundi haya, na pia kujitathmini:-
Wafanyakazi
Hawa ni waajiriwa na hawako tayari kujiajiri, kama watajiajiri labda ni kwa sababu wamekosa kazi ya kuajiriwa. Na hata kama wakianzisha biashara, na baadaye kusikia sehemu fulani kuna kuajiriwa kwa mshahara mkubwa, wataiacha biashara na kwenda kuajiriwa. Kama upo kwenye hili kundi, unatakiwa ujue kuwa wewe sio mfanyabiashara. Ata kama utaanzisha biashara ni kwa sababu kazi ya kuajiriwa haipo. Na mara nyingi hili kundi halijui mikikimikiki ya biashara.
Wafanyabiashara
Hili ni kundi ambalo watu wake hutafuta fursa na kuanzisha biashara inayolipa kwa muda uliopo, wakiona biashara hii hailipi, wataamia kwenye biashara nyingine inayolipa. Mara nyingi kundi hili, linaangalia bidhaa inayohitajika kwa wakati uliopo sokoni.
Wachuuzi
Hawa ni wafanyabiashara ndogo ndogo, wanaofanya ili waweze kupata mahitaji yao ya kila siku. Wanakuwa na mitaji midogo midogo. Na watu wengi wapo kwenye hili kundi. Wengi wanaingia na kutoka.
Wajasiriamali
Ili kundi linabeba wabunifu mbalimbali ambao hawako tayari kuajiriwa. Ata kama utawalipa mshahara wa milioni 50 kwa mwezi hawaajiriki. Ni kundi linaloamini kile wanacho kitazamia. Wako tayari kukaa kwenye biashara yao hata kama anapata hasara, lakini kuna kitu amekilenga baada ya muda fulani lazima jamii itambue mchango wake.
Kujua kundi uliopo, litakusaidia katika kujipanga kwa kile unachotaka kukianzisha.