Unatakiwa uwe na shilingi ngapi ili ufanye ujenzi wa nyumba?

Unatakiwa uwe na shilingi ngapi ili ufanye ujenzi wa nyumba?

Alvin Slain

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
6,375
Reaction score
3,663
Habari wakuu.

Naomba kufahamishwa kama nataka kufanya ujenzi wa nyumba ya vyumba viwili kimoja master kingine cha kawaida, Bafu na choo la public, Jiko, Sebule na dining. Je, niandae shilingi ngapi niweze kuhamia ndani.

Karibuni
 
Sina uzoefu sana,ila itategemea na ukubwa wa hiyo nyumba yenyewe na utataka iwe ya design gani...
 
Una mahali pa kufanya ujenzi tayari? Eneo.
Una ramani/mchoro?
Unatarajia kutumia wataalam au "fundi Japhet/Juma".?
 
Eneo/Kiwanja ninacho tayari Mkuu.
Ila ramani sina vile vile fundi ntatafuta wakati nikikamilisha hatua ya kujua garama zake
Depending na eneo husika, kwa uhitaji huo jiandae na 13.5 mil Tsh na kuendelea kulingana na finishing utakayotaka na utakayomudu.
 
Depending na eneo husika, kwa uhitaji huo jiandae na 13.5 mil Tsh na kuendelea kulingana na finishing utakayotaka na utakayomudu.
Unaweza kuoanisha hapa huo mchanganuo wa 13.mil Tsh Mkuu?
Asante
 
Inategemea hupo Mkoa gani ila kwa haraka haraka uwe na million 10

Mi nakumbuka nilianza ujenzi nikiwa na buku yaani shilingi elfu 1 ,lakini mpaka sasa nimefanya ujenzi wa 12 million na sikuwa na haraka ya kuhamia
Mkuu ulianza kujenga kwa elfu 1!
hii yako kama zile za motivational speakers, nilianza biashara ya kuku nikiwa na nyoya moja (mr kuku)
 
Inategemea hupo Mkoa gani ila kwa haraka haraka uwe na million 10

Mi nakumbuka nilianza ujenzi nikiwa na buku yaani shilingi elfu 1 ,lakini mpaka sasa nimefanya ujenzi wa 12 million na sikuwa na haraka ya kuhamia
Motivational speaker....anyway itakuwa ilikuwa mwaka 1960
 
Sasa mkuu si itategemea na unajenga nyumba ya aina gani na kwa mtindo upi.
 
Back
Top Bottom