Unatumia Mbinu gani kuimarisha Usalama wako Mtandaoni?

Unatumia Mbinu gani kuimarisha Usalama wako Mtandaoni?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Imarisha Usalama wako Mtandaoni kwa kufanya yafuatayo;

a. Sasisha (Update) Kivinjari chako kila linapotoka toleo jipya. Unaweza kuruhusu Kivinjari kiweze kujisasisha 'automatically'

b. Tembelea tovuti zenye alama ya ‘kufuli’ au zenye 'HTTPS'

c. Pakua majalada (files) au Programu Tumizi (Apps) kwenye vyanzo vya kuaminika kama 'PlayStore' au 'AppStore'

d. Usikubali ‘cookies’ bila kusoma na zifute mara kwa mara ili kuzuia ufuatiliaji wa shughuli zako

e. Zuia matangazo ili kuimarisha usalama wako wa faragha mtandaoni

f. Tengeneza Nywila (Password) imara na wezesha uthibitishaji wa hatua Mbili 'two-factor authentication'

g. Zuia ufuatiliaji wa shughuli zako za mtandao kwenye tovuti
 
•Usibonyeze link kutoka kwenye chanzo usicho kielewa au unachokitilia mashaka

•Usigawe sim yako ovyo watakunyoosha.

• Usi save passwords kwenye kivinjari
 
Back
Top Bottom