lorahshop
Member
- Oct 16, 2021
- 39
- 69
Miswaki ni mingi, mimi ninatumia colget na mingine haina jina ya kichinachina.Inauzwa kwenye maduka yanaitwa Litle more.
Kuwa makini: Nimeona unasema unataka ukipiga mswaki meno na fizi viitikie. Japo sijajua unamaanisha nini hasa,lakini, nakutahadharisha kuepuka miswaki yenye brashi ngumu kupitiliza. Hakikisha brashi zinaweza kulala unapotumia. Kuna miswaki hata ile ya gharama,migumuu utasema ya kusugulia sakafu. Hiyo haifai. Shida kubwa ya brashi ngumu na kutumia nguvu ni kwisha kwa tabaka la juu la meno(enamel, sijui kama nimepatia).
Enamel ikiisha, utaanza kupata tatizo la sensitivity. Hapo utasahau ukoko wa ubwabwa, kitumbua kilichokauka, nyama iliyokauka na usilogwe utafune kamfupa ama jiwe.Hata mtu akikikwangua ama kukereza kitu ,mfano, msumari juu ya sakafu ,kraaaaaaaaaah! utakoma. Mimi ni victim wa tatizo hili,hivyo, sasa nimekuwa mpole,ninatafuta miswaki bora na laini.
Little more wana vitu vizr sana