Afrika yetu sote
Member
- Jun 12, 2022
- 5
- 8
Watu wengi huwa tunaomba ushauri kwa watu mbalimbali ili watusaidie pale tunapohitaji, lakini ikitokea tumegombana na wale waliotupa ushauri, tunazikuta siri zetu nje ya hapo.
Sasa wewe unatumia njia gani kumpata mshauri anayefaa?
Kuna baadhi huwa tunawachukua marafiki kama washauri ila kibaya ni kuwa kuna mambo huyavutia kwake, yaani kama unamshirikisha kuhusu mahusiano yako na kumbe yeye anampenda mwenzako, hivyo unaweza kujikuta amekupa ushauri ili muachane ili yeye aingie.
Na baada ya hapo anaweza kutumia kusema siri zote ulizokuwa unamwambia kuhusu mpenzi wako, na anajikuta anatengeneza uadui na mpenzi wako.
Unatumia njia gani kumpata mshauri?
Mimi ili mtu anishauri huwa napenda kuangalia vitu vifuatavyo:-
A. Ujuzi wake kwenye masuala ninayohitaji ushauri.
B. Kama mtu ameshawahi kupitia hilo ninalopitia. Kwani watu wanavyokupa wewe ushauri huwa wanajiongelea wao kuhusu mambo waliyopitia
C. Kifua cha kuficha mambo, kama ni rafiki yangu na ananipa ushauri nitaangalia je huwa ananiambia kuwa nani na nani aliwashauri, kama huwa ananipa siri za wengine siri zangu siwezi kumwambia acha niubebe mzigo wangu.
D. Mwanasaikolojia wa suala husika, kama shida yangu ni ya kisaikolojia basi nitatafuta mshauri mwenye uwezo wa kushauri kisaikolojia.
Rafiki pekee uliyebaki naye ni yule adui yako, maana rafiki yako ni adui yako ajae...
Vijana tuepuke kutoa siri za wapenzi wetu kwa marafiki zetu, usimshirikishe kila kitu rafiki yako, angalia uwezo wa kutunza siri.
Ni bora kuonekana mbaya kwa mwanzo lakini huku umemfichia siri mpenzi wako.
Kuna mahusiano yanakufa mapema kwa sababu mpenzi anatangazwa kwa marafiki zake.
Kila mtu ana agenda za siri sehemu yoyote.
Sasa wewe unatumia njia gani kumpata mshauri wa mambo yako na anayekubebea siri?