Unatumia njia gani kuwasaidia ndugu na jamaa zako pale kipato chako kinapokuwa chini ya mahitaji yako ya muhimu?

Jamii zetu ni watu wa kupenda kusaidiwa sana wanapoona ndugu au jamaa anapokuwa na kipato cha uhakika lakini cha ajabu mbongo hana moyo wa kutoa msaada wala mazoea ya kutoa msaada hata chembe nilivyokuwa chuo nilishuhudia ndugu zangu wa karibu kabisa,jambo la msingi ni kuishi kama wazungu mzazi,wanao na mkeo akina dada,dogo kama amemaliza chuo,mjomba sijui nani huko wapambane na hali zao kama mimi sikupata msaada kwa mtu yoyote kwanini isiwe kwao.
 
Ha ha haa. Unyama unyama tu, au siyo? Kwa maoni yangu nadhani kama una nafsi ya kusaidia inakubidi usaidie tu bila kujali kama ulisaidiwa ama la. Lazima ujue ndani ya dhamiri yako kuwa kwanini inakubidi kusaidia na unalenga ku-achieve jambo gani katika maisha yako ili uishi kwa furaha. Kama moyo wako unafurahia kufanya jambo hilo ni vema ukafanya, kama haufurahii unaweza kuacha pia.
 
Kwa upande wangu naona ni vema kusaidia kwa uwezo wako ila si kila saa ili usigeuke tegemezi kwa asilimia 100.

Hili ni jambo ambalo nafanya kwa ndugu wote wanaoniomba pesa. Kuna mida nakupa yote. Kuna mida nakupa nusu. Kuna mida sikupi kabisa.

Nachanganya hivi ili nisije kujulikana kama mtu toatoa hela asiyejua kusema hapana katika ukoo/familia jambo ambalo nasikitika linaleta mzigo sana kwa wengi kwenye familia za kiafrika. Hivyo unakuta nikiingia katika mode ya NO inapita miezi sijatoa hela kwa ndugu labda tu pesa ambayo naitoaga automatically kwa mama kila mwezi kusaidia expenses zake.
 
Manka kama Manka
 
Saidia wanaokusaidia mkuu,Chuma huliwa na chuma,dawa ya moto ni moto. Mimi ndugu hawajawahi kunisaidia,so kamwe sitowasaidia ila wahuni tu wa mitaani wamenisave sana kipindi nahangaika.

Ndio maana niko tayari nimsaidie mtu baki ila sio ndugu[emoji51][emoji51][emoji51]
 
Msaada ni kama sadaka, toa kwa moyo na kile ambacho unauwezo nacho, msaada usizidi kipato.
Ningejua kama wewe ni mfuasi wa BIblia ningeweza kukuuliza hapo kwenye kutoa usizedi uwezo, vipi kuhusu kuhusu sadaka ya yule mama Mjane aliyetoa senti yake ya mwisho kabisa?
 
Ningejua kama wewe ni mfuasi wa BIblia ningeweza kukuuliza hapo kwenye kutoa usizedi uwezo, vipi kuhusu kuhusu sadaka ya yule mama Mjane aliyetoa senti yake ya mwisho kabisa?
Mimi ni mfuasi wa upande mwingine.
 
Umeongea kweli ila mkuu si kila ndugu wako ivyo.

Kuna watu wanasaidiwa na marafiki zao kuzidi hata hao ndugu.

Labda tuseme hivi, pale tunapoweza tusaidie bila kujali ni ndugu ama rafiki. Kila mtu katika maisha yetu ana mchango wake. Tuwape nafasi kwa kiasi . Tusije kuamini sana ndugu tukasahau marafiki. Imagine mtu unaishi Dar es Salaam na ndugu wako Kigoma itakuwaje siku umekwama , mgonjwa taabani utasaidiwa na nani????

Binafsi nawajali wote kadri ya uwezo wangu.!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hili suala la " kusaidiana" lipo overrated Sana katika jamii za kiAfrika.Tatizo Ni pale unapojitoa kuwasaidia watu/ mtu fulani ukitegemea itafika siku fulani waanze kujisimamia na kujikimu wenyewe,kumbe wao Wala hawajistukii ila wanaendelea kukutegemea siku nenda siku Rudi.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…