Unatumia njia gani kuwasaidia ndugu na jamaa zako pale kipato chako kinapokuwa chini ya mahitaji yako ya muhimu?

Hili andiko Lina ukweli asilimia πŸ’―
 
Kutoa msaada unao mudu hakuna tatizo kabisa. Lakini msaada unatoa wa aina gani?

Nadhani ni pamoja na msaada wa mawazo au ushauri.

Kuna wapokea misaada na kuamini wataishi kwa kupokea misaada.

Nadhani hakuna misaada ya kudumu. Mtu apatapo msaada afikirie pia namna ya msaada utakavyo mfanya ajitegemee.

Sidhani kama ni sahihi kuamini kuwa duniani wameumbwa wa kutoa misaada na wa kupokea misaada.

Kuwaza kwa namna hiyo kunaendekeza jamii kufikiria kuwa wapokea misaada zaidi badala ya kufikiria kuwa watoa misaada.
 
Ujinga wa kusaidia ndugu staki kuuskia kabisaaaa, kumsaidia ndugu ni kuzidi kulimbikiza umaskini
 
Hali unayopitia tunapitia wengi wenye moyo wa kuwasaidia wengine, changamoto ndiyo hiyo hiyo! Binafsi naweza kujinyima ama kupunguza standard yangu ya maisha kwa ajili ya mzazi wangu au mkwe wangu tu, hawa wengine itategemea sana na uhitaji alionao, huwa siwapi kipaumbele sana kiasha cha kujinyima na kupunguza mahitaji yangu muhimu kama vile kupunguza kilo za mchele, unga n.k kwa ajili yake. Naamini wao wanazo nguvu kama wakiwa na bidii ya kujishughulisha pasipo kuchagua kazi lazima watapata kipato cha kujikimu. Zaidi ya hapo labda nikipata cha ziada ninachoqeza kufanya saving ama uwekezaji, hicho naweza kumega kidogo nikamsaidia ndugu/jamaa ya karibu mwenye shida yake. Ila kwa mzazi ama mkwe wangu hapo sina namna hata kwa kukopa nitakopa atatue shida yake na mara nyingi hawa huwa hawana anasa kiasi cha kulemea.
 
Safi sana, kama nafasi inaruhusu sawa kama hairuhusu basi
 
Ukweli mtoa mada nimeuelewa uchambuzi wako!

Hali katika jamii zetu inatisha,
Umeajiriwa/umejiajiri lakini huwezi hata kumudu mahitaji yako yote ya msingi,bado wategemezi.Sasa bado wale waliokusaidia/ndugu zako!

Mwisho simu ikiita roho inaanza kudunda ukidhani ni yule ndugu yako uliyemuahidi kiasi flani cha pesa mwisho wa mwezi,hali inaendaaaa mpaka unasindwa kutimiza ahadi zako zilizonyingi,

Nini kinatokea,unasajili laini mpya ya simu kisha unaitambulisha kwa baadhi tu ya wale wanaokuelewa/wanaoelewa hali yako na kukuvumilia!

Ama unauchuna kabisa lakini huku ukiugulia maumivu ya kukaa mbali na jamaa zako!
 
Ndio muanze kuelewa na kuwafundisha watoto wenu, kuwa ndugu ni wa familia moja tu...
Si cha binamu, wala mjomba....
Mimi nimeishi maisha ya utotoni nikiona ndugu wakipishana kwetu, mpaka inabidi tunalala wawili au tunatandika carpet chini tuwaachie mara ndugu upande wa baba mara wa upande wa mama ili walale kwenye vitanda, mpaka Mama alichoka baadae lakini hawaishi...
Baadae Mdingi alivyostaafu, walipotea kama pata potea ya mazingaombwe, tulijikuta tupo familia moja wenyewe tu na mpaka tulifikia asubuhi ni chai ya rangi tu imetoka hiyo...na msosi ni mmoja kwa siku.
Ndio tukajifunza, na kuelewa, na baadae tukajipanga wote kila mmoja wetu anaendesha familia yake binafsi na kujiweza kimaisha above average na bila kumsahau Mama yetu kipenzi aliyebaki...
Sasa picha linaanza upya...wale waliokuwa wanakuja home na wakapotea baada ya Mzee kustaafu, sasa watoto wao ndio wanatutafuta kuendeleza ule mtindo ule ule, hapo unakuta wanaambiwa na wazazi wao, hao kina fulani ni ndugu zenu wafuateni wawasaidie....
 
We jamaa unaonekana unamoyo na malengo mazuri ya kuwasaidia ndugu zako na unaonekana unalaumiwa sana na ndugu yaani kiufupi ulichokiandika kinakuelezea wewe. Pole sana.
Tutafute pesa ayseee kazi za kuajiliwa ni kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani tu zaidi ya hapo ni majanga.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hongera sana
 
Uliyo yasema karibu yote yamenigusa direct ....in real life ....unajua wakati mwingine unaweza inekana una maisha mazuri kulingana na familia zetu zinavyo ishi kule kijijini lakini katika uhalisia siyo kweli ..... mmi kwa upande wangu kuna mda najinyima kiasi flani kisha namtumia maza siyo rahisi sana ila walau kila mwezi namyumiaga walau kidgo na huwa ananishukuru sana japo huwa naona ni kidgo ..... kutoa ni moyo tujitahidi kujinyima walau kwa kiasi tukumbuke ndugu au wazazi
 

1. Kwenye Maisha usifanye kitu Kwa kuogopa lawama.
Fanya kitu moyo ukiwa unataka/penda kufanya.
Utumwa wa maisha ni Mbaya.

2. Kuwa tegemezi pekee ni ubinafsi namba moja. Hao wanaosema MTU Fulani ni mbinafsi Kwa sababu hawasaidii wao ndio wabinafsi Square.

3. Saidia pale unapoweza na vile upendavyo na sio vinginevyo.
Kusaidia ni hiyari sio lazima. Ni ishu ya upendo.
Wanaolazimisha kusaidia ni wabinafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…