Unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi?

Unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi?

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Heshima yenu wadau.

Nimekaa muda huu nikakumbuka kifungua kinywa changu. Nimekula vitumbua 10 na supu ya utumbo.

Kitumbua kimoja shilingi 100 hivyo nimetumia 1000 kwa ajili ya vitumbua. Supu ni 500.
Jumla asubuhi nimetumia 1500.

Mwenzangu unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya asubuhi?
 
Wapendwa usiangalie mwenzio kala nini na wewe uige, angalia mwili wako unahitaji nini kwa wakati gani? Hatulingani afya zetu, usione mwenzio anafakamia starch kumbe mwili wake unahitaji hio zaidi. Ukiiga anayefakamia protini wakati wewe kwako zimezidi pia ni matatizo.

Chunguza mwili wako unahitaji nini ndo ule, kama husikii njaa usile kabisa ujue siku hiyo mwili unatumia akiba yake ya mwili.

Kasie Mahaba mpenda Misosi Yote!!😉
 
Mh kwa hiyo asubuhi na mchana unaimaliza kwa 500. Optimization succeeded
Kwani husomi alama za nyakati.....serikali ikibana matumizi ...na raia inabidi abane matumizi ili ku-equate mambo
 
Wapendwa usiangalie mwenzio kala nini na wewe uige, angalia mwili wako unahitaji nini kwa wakati gani? Hatulingani afya zetu, usione mwenzio anafakamia starch kumbe mwili wake unahitaji hio zaidi. Ukiiga anayefakamia protini wakati wewe kwako zimezidi pia ni matatizo.

Chunguza mwili wako unahitaji nini ndo ule, kama husikii njaa usile kabisa ujue siku hiyo mwili unatumia akiba yake ya mwili.

Kasie Mahaba mpenda Misosi Yote!!😉
Hahaha 'Mpenda misosi yote'

Uzi ni kwaajili ya info tu. Hauna lengo la kusababisha mtu amuige mtu. Kwahiyo mpenda misosi tuibie hiyo siri ya asubuhi
 
Back
Top Bottom