Unaujua ugonjwa wa minyoo ya mbwa???, kitaalamu unaitwa HYDATIDOSIS

Unaujua ugonjwa wa minyoo ya mbwa???, kitaalamu unaitwa HYDATIDOSIS

MIDFIELD

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Posts
1,944
Reaction score
702
Je, unajua Hydatidosis?

Kwa kifupi ni ugonjwa unaomuathiri binadamu na wanyama tunaowafuga kama ng'ombe, kondoo na mbuzi. Ugonjwa huu huathiri zaidi maini, mapafu, moyo, bandama na wakati mwingine hata ubongo na mifupa kotekote kwa binadamu na wanyama niliowataja (ruminants). Mwambukizaji mkuu wa ugonjwa huu ni mbwa.

Hebu angalia kidogo sehemu ya ini iliyoathiriwa ya mbuzi na ng'ombe. Hiyo ni sehemu ya utafiti wangu nilioufanya Dodoma juzi kati
, tatizo ni kubwa kwa wanyama, na hii ni ishara kwamba hata kwa binadamu tatizo lipo katika jamii zetu ila watu wanaugua bila kujua anaumwa nini. Matokeo yake mtu anaweza kupoteza maisha, halafu tukabaki kusingizia ushirikina.

Tuamke tuzuie Hydatidosis (minyoo ya mbwa).

Jamani kwa wale msionijua ni nafasi yenu kuniona. Hapo mwenye yellow cap
 
Haya tushakuona mkuu…sasa ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia gani ya hewa,kinyesi,ukaribu na mbwa?Ni virusi,bacteria,parasite?na tiba yake ni ipi?Dalili zake ni zipi,na diagnosis inachukuliwa na vipimo gani?Kuna vipimo vyovyote vinavyoweza kuthibitisha mtu ameadhirika na ugonjwa huu?
 
Nashukuru sana kama umeona. Majibu yako ni kama ifuatavyo: Ugonjwa unasababishwa na minyoo wanaoitwa Echinococcus granulosus wanaopatikana kwa mbwa (definitive host).

Mayai ya hii minyoo hutolewa pamoja na kinyesi cha mbwa na hivyo kucontaminate majani, maji, udongo na mboga ambavyo wanyama hasa ng'ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe na hata binadamu (intermediate hosts) wanaweza kula na kupata cysts hasa kwenye maini na mapafu kama zinavyoonekana kwenye picha za mleta mada.

Mbwa akila maini au mapafu ya wanyama yalio na hizo cysts, ile minyoo iliyo kwenye hizo cysts inakamilisha hatua zake za ukuaji katika utumbo wa mbwa kutengeneza minyoo ambao hutoa mayai na hivyo mzunguko kujirudia. Kwa binadamu cysts inaweza kuwa kubwa na kuathiri utendaji kazi wa viungo muhimu kama ini na endapo itapasuka inaweza kusababisha hata kifo.

Kuzuia huu ugonjwa ni kuzingatia tahadhari muhimu za afya kama kuchemsha maji na mboga za majani na kuosha matunda ili kuondoa uwezekano wa kula mayai ya hii minyoo.

Pia kwa wale wanaocheza na mbwa, mfano, pet dogs kunawa mikono ili kuzuia uwezekano wa kuambukizwa mayai ya hii minyoo kutoka kwa mbwa, mbwa wapewe dawa za minyoo routinely, zuia tabia ya kuwatupia mbwa nyama isiyochemshwa hasa maini na mapafu yaliyo na cysts.

Dalili za ugonjwa huu kwa binadamu itategemea hiyo cyst imejikita wapi. Mfano kama ni katika mapafu, mgonjwa atakuwa na dalili zifuatazo:

-kukohoa mara kwa mara kwa muda mrefu bila kujua sababu

-kifua kuuma na wakati mwingine kupata tabu kupumua

Na ikiwa cyst ipo ktk ini, mgonjwa atavimba tumbo kadiri cyst inavyokua, maumivu sehemu za tumbo, n.k.
Na kama cyst ikipasuka maji yake yakamwagikia ndani ya mwili, basi mgonjwa hupata allergy kali sana, na anaweza hata kupoteza maisha. Cha kuzingatia, madaktari wachache sana wanaoweza kugundua hili tatizo.

T
iba yake kwa binadamu ni:

1. Kama inawezekana ni kufanyiwa upasuaji kuondoa hiyo cyst katika kiungo ilipo

2. Kama cyst ni nyingi, upasuaji hauwezekani, hivyo utatumia dawa za minyoo kwa muda mrefu ili kuwaua hao minyoo. dawa zenyewe ni Albendazole au Mebendazole.

Kwa mbwa inabidi apewe Praziquantel kuua hao minyoo

Diagnosis yake ni kwa

Xray, CT-Scan, Ultrasound au MRI. Lakini pia unaweza kuhakiki (confirm) kwa serology kwa ELISA au vipimo vinavyoweza kuonesha antigens ktk damu ya mgonjwa.
 
Nashukuru sana kama umeona. Majibu yako ni kama ifuatavyo:
Ugonjwa unasababishwa na minyoo wanaoitwa Echinococcus granulosus wanaopatikana kwa mbwa (definitive host), mayai ya hii minyoo hutolewa pamoja na kinyesi cha mbwa na hivyo kucontaminate majani, maji, udongo na mboga ambavyo wanyama hasa ng'ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe na hata binadamu (intermediate hosts) wanaweza kula na kupata cysts hasa kwenye maini na mapafu kama zinavyoonekana kwenye picha za mleta mada. Mbwa akila maini au mapafu ya wanyama yalio na hizo cysts, ile minyoo iliyo kwenye hizo cysts inakamilisha hatua zake za ukuaji katika utumbo wa mbwa kutengeneza minyoo ambao hutoa mayai na hivyo mzunguko kujirudia. Kwa binadamu cysts inaweza kuwa kubwa na kuathiri utendaji kazi wa viungo muhimu kama ini na endapo itapasuka inaweza kusababisha hata kifo.
Kuzuia huu ugonjwa ni kuzingatia tahadhari muhimu za afya kama kuchemsha maji na mboga za majani na kuosha matunda ili kuondoa uwezekano wa kula mayai ya hii minyoo, pia kwa wale wanaocheza na mbwa, mfano, pet dogs kunawa mikono ili kuzuia uwezekano wa kuambukizwa mayai ya hii minyoo kutoka kwa mbwa, mbwa wapewe dawa za minyoo routinely, zuia tabia ya kuwatupia mbwa nyama isiyochemshwa hasa maini na mapafu yaliyo na cysts

Dalili za ugonjwa huu kwa binadamu itategemea hiyo cyst imejikita wapi. Mfano kama ni katika mapafu, mgonjwa atakuwa na dalili zifuatazo:
-kukohoa mara kwa mara kwa muda mrefu bila kujua sababu
-kifua kuuma na wakati mwingine kupata tabu kupumua
Na ikiwa cyst ipo ktk ini, mgonjwa atavimba tumbo kadiri cyst inavyokua, maumivu sehemu za tumbo, n.k.
Na kama cyst ikipasuka maji yake yakamwagikia ndani ya mwili, basi mgonjwa hupata allergy kali sana, na anaweza hata kupoteza maisha.
Cha kuzingatia, madaktari wachache sana wanaoweza kugundua hili tatizo.
T
iba yake kwa binadamu ni:
1. Kama inawezekana ni kufanyiwa upasuaji kuondoa hiyo cyst katika kiungo ilipo
2. Kama cyst ni nyingi, upasuaji hauwezekani, hivyo utatumia dawa za minyoo kwa muda mrefu ili kuwaua hao minyoo. dawa zenyewe ni Albendazole au Mebendazole.

Kwa mbwa inabidi apewe Praziquantel kuua hao minyoo
Shukraan kwa somo hili….
 
Back
Top Bottom