Unauonaje mwenendo wa klabu ya Simba kimchezo chini ya Kocha Sven Ludwig Vandenbroeck?

Unauonaje mwenendo wa klabu ya Simba kimchezo chini ya Kocha Sven Ludwig Vandenbroeck?

Kuna aina ya ulalamikaji, kibaya zaidi viongozi wa timu hizi kariakoo wanasikiliza sana maneno ya mashabiki badala ya kufanya kazi zao kwa kuzingatia misimamo yao. Mashabiki walivyopiga kelele nyingi za hatumtaki uchebe na chupa wakamrushia kisa tu matokeo ya mechi moja kupoteza na sare moja kilichofuata ni kweli Uchebe kafungashwa virago.

Hivi sasa mashabiki waliona waliona ni kosa kubwa ulifanyika kumfukuza uchebe pasipo kukumbuka hisia na mihemko yao ndio yaliyopelekea hayo yote.

Kwahiyo kwa Sven, hayo matatizo hayo ulioanisha ni sahihi kwake kutimuliwa baada ya kufungwa na Polisi Tanzania?

Kwa kweli angeng'ang'ani mfumo wake mshambuliaji mmoja naamini hata wewe kama ni shabiki wa Simba uvumilivu ungekushinda. Sina uhakika kama ulitazama mfululizo wa mechi kuanzia Simba dhidi ya Mwadui, Namungo,Polisi na JKT Tanzania. Kiwango cha Simba kiliporomoka kwa kasi ya ajabu sana. Kwa wachezaji waliopo Simba sio timu ya kuanza kusubiri kufungwa na kuanza kutafuta kusawazisha dakika za mwishoni na kutafuta ushindi dakika za majeruhi. Kiukweli katika hizo mechi nne Simba ilicheza kama timu iliyojikusanya mtaani bila hata kuwa na kocha na kilichoikoa kwenye hizo mechi tatu za mwanzo kati ya nne ni marefa na washika vibendera vinginevyo huyo Sven hata mechi na Mtibwa asingefika.

Kocha mzuri ni yule anayekubali kubadilisha mbinu zake mara kwa mara iwapo anaona hakuna mafanikio kwa mbinu fulani anazotumia. Kwa Sven amechelewa sana kubadili mbinu zake.
 
Shida mashabiki wengi hawajui kuangalia mpira kiufundi, Simba mechi zote alizoanza kucheza vibaya sio kwa sababu ya kushindwa kwa mbinu za kocha, angalia bao la jkt goli linafungwa Wawa yupo hapo hapo. Simba ilikua inashindwa kwa sababu ya viongozi kushindwa kutatua mgogoro ambao ulikuwepo kati ya hao makocha wa simba, mbinu za mwalimu zilikua zinafanya kazi ila wachezaji walikua hawajitumi uwanjani. Hata kama una mbinu nzuri sana kama umekosa juhudi ya wachezaji haziwezi kufanya kazi.
Simba ilikua na performance mbovu kwa sababu ya wachezaji kutokujitolea uwanjani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom