Unavyonunua gari fikiria na uwezekano wa kupata mteja kama ukiamua kuliuza

Unavyonunua gari fikiria na uwezekano wa kupata mteja kama ukiamua kuliuza

Hizo ambazo haziuziki mngelizitaja haswa Toyota brand, mgetisha sana. Ukizingatia kwa takwimu bongo tunatumia sana Toyota.
 
Kuna magari ni kama "mimba" (tukumbuke umri wa mimba isiyo na hitilafu ni siyo chini ya miezi tisa).

Kuna magari hayauziki hata upunguze bei kiasi gani labda uuze kwa hasara kubwa au uuze kama skrepa lakini kuna magari mengine unaweza kupata mnunuzi wa bei nzuri tena siku hiyohiyo unayotangaza kuuza.

Tuwe makini wajameni maana inachanganya sana unapotaka kuuza hlf wateja hawatokei au wanayeyuka ghafla.

usiseme hujaambiwa.
Nani alikwambia kila anaenunua gari anawaza kuliuza baadae?
 
Mkuu hakuna gari isiyo na spare. Siku hizi unaweza kuagiza spare UK, Dubai au China ikakufikia Ndani ya week.
Changamoto ni kwamba wengi tunanunua magari yaliyochoka. Ununue discovery 4 kwa Mzee wa madungu Jeshi yenye miaka 15, wewe uitumie kwa miaka 5 au 7 then utake Kuuza kwa faida? Shida inaanzia hapo. Ndo maana malalamiko dhidi ya magari ya Ulaya hayaishi.

Nunua gari ya 2020, utumie hata miaka saba uone kama utapata shida kuuza.
Jidanganye hivyo hivyo, as long as gari uliyonunua 2024 imesajiliwa leo kwa namba "EK" basi baada ya miaka saba namba zitakuwa zipo kwenye series ya "F" hio gari yako utauza kwa bei ya nyasi balaa.
 
Umeongea point muhimu sana. naonaga jamaa wananunua ma discovery kwa mzee wa madungu nawaonea huruma sana; tena hiyo mika mitano umesema ni ming sana. Discovery has za UK ikivuka mileage 100k hayo ni maumivu makubwa ukiichukua, utajuta
Stori za vijiwe vya kahawa hivi. Yaani IST ilovuka mileage 100k isilete maumivu halafu Discovery yenye injini kubwa ikupe maumivu kwa hizo kilomita chache? Au we mgeni kwenye magari jombaa. Tatizo la wabongo ni service tu wala si mileage ndio shida. 100k mileage ni ndogo sana kwa madungu..tatizo wabongo service za kuunga afu wanaishia kulaumu brand
 
Mkuu hakuna gari isiyo na spare. Siku hizi unaweza kuagiza spare UK, Dubai au China ikakufikia Ndani ya week.
Changamoto ni kwamba wengi tunanunua magari yaliyochoka. Ununue discovery 4 kwa Mzee wa madungu Jeshi yenye miaka 15, wewe uitumie kwa miaka 5 au 7 then utake Kuuza kwa faida? Shida inaanzia hapo. Ndo maana malalamiko dhidi ya magari ya Ulaya hayaishi.

Nunua gari ya 2020, utumie hata miaka saba uone kama utapata shida kuuza.
Swala la kuagiza spea lisikie tu kwa mwenzio, sio kitu rahisi na wala msidanganyane, unaweza kuagiza spea ikatumia wiki ukaja kulipa kodi kibao halafu kwenye kufunga ngoma inanaonekana ni tofauti, back to square one, watu wanapenda gari za japan maana spea zipo mjini hapa hata ikiletwa tofauti ni swala la boda tu chap inabadolishwa
 
Usinikumbushe discover 3 mkuu

Tangu 2018 nmetangaza kuuza Kwa madalali wote unaowajua mjini Ila HOLA.

Nmekuja kuiuza Kwa msukuma mmoja mwaka jana, Tena kwny mnada WA mifugo Kwa exchange na ng'ombe+Ela kidg😡
Hasa mikoani ndo unaweza usiuze kabisa. Bora Dar vijana wanajilipua tu kutengeneza majina ndio maana madungu saizi kila kona,usishangae in two years ukaja ambiwa ndio brand inayoongoza kununuliwa Dar maana jamaa zangu kibao wanaswitch huko hadi namimi nishakua na mawazo ya kuingia kwenye madungu 'kazi ni kipimo cha utu '
 
pole sana ,
mimi huwa nazingatia ulaji wa mafuta na gharama za maintance .Pia lisiwe gari la chini sana.Lisiwe linakula mafuta sana kuliko uwezo wangu,lisiwe na gharama kubwa za matengenezo kuliko uwezo wangu,lisiwe la chini sana au ambalo haliwezi kupita baadhi ya barabara.
SIJAWAHI JUTIA kununua gari hii TOYOTA RAV 4 OLD MODEL ya 1996
Namba A safi engine ya 3s au nadema uwongo😁
 
Back
Top Bottom