Unawafahamu wanawake wa Amazon?

Unawafahamu wanawake wa Amazon?

Umewahi kuitazama muvi ya Wonder Woman iliyochezwa na mwadada Gal Gadot? Ni muvi inayohusu wanawake Fulani wanaofahamika kama Amazon Women.

View attachment 2600628

Kwa mujibu hadithi za uhiriki (Greek mythology) zinasema kwamba Amazon Women walikua ni jamii ya wanawake ambao walikua hatari sana katika medani za kivita. Walikua wana nguvu hawakua wakiishi na wanaume bali walikutana na wanaume mara moja tu kwa mwaka ambapo walitumia nafasi hiyo kubeba mimba, kama mtoto alipatikana mwanaume basi walimrudisha kwa baba zao na kubaki na watotoo wa kike tu amabao waliwafundisha na kuwaandaa kua wapambanaji.

Wanawake hawa walisifika kwa kupiga mishare na kuendesha farasi, walikua na tabia ya kukata maziwa yao ndio maana walikua hodari katika kupiga mishale, Kwakua walikua wanawake watupu inasemekana hawa walikua hodari wa kusagana pia…lakini pia kwa makabila mengine ya hawa Amazonian walikua na tabaia ya mwanamke mmoja kua na wanaume hadi wanne.

Kuna jamaa mmoja kutoka Hispania anaitwa Francisco de Orellana alikua anafanya uchunguzi wake huko kwenye mssitu wa brazil, alipokua kwenye mto mkubwa unaopatikana katika msitu huo alikutana na jeshi la wanawake watupu wakiwa kando yam to huo. Hivyo akauita mto huo Amazon kutokana na wanawake hao walifanana na wale wanawake wa kwenye simulizi za kigiriki. Lakini pia hata msitu huo ulianza kufahamika kama Amazon kutokana na jina la mto huo…na hicho ndio kikawa chanzo cha msitu mkubwa duniani uliopo Brazil kuitwa Amazon.

View attachment 2600602

[Amazon women as depicted in Wonder Woman film]

Katika karne ya 17 huko Africa magharibi kulikua na falme iliyojulikana kama Kingdom Of Dahomey ambayo kwa sasa inafahamika kama Benin, ilikua falme yenye nguvu sana kutokana na biashara ya mafuta ya mawese na biashara ya watumwa. Walipa wazungu watumwa wao wakapewa bunduki, vioo, nk. Falme hii ilikua ina jeshi la wanawake watupu ambao walikua imara kwelikweli na wapiganaji mashuhuli waliojulikana kama Dahomey.

Kikawaida tamaduni za kiafrika tunamchukulia mwanamke kama kiumbe duni na dhaifu, ilikuaje wanawake wakaingizwa jeshini? Kutokana na vita mbalimbali zilizokua zikitokea baina ya falme na falme zilipelekea wanaume kupungua pia wanaume wengi waliuzwa kama watumwa hivyo population ya wanaume ikawa ndogo. Ndio hapo wafalme wa falme ya Dahomey wakaanza kuchukua wanawake na kuwatumia kama wanajeshi wake. Jeshi hilo la wanawake watupu lilijulikana kama Agojie, unaambiwa walikua ni hatari sana kwenye mapigano..Wazungu walipowaona wakawapa jina la Dahomey Amazons

wakiwalinganisha ushupavu wao na wale wanawake kutoka kwenye hadithi za wagiriki. Dahomey ilikuja kuanguka mwaka 1890 kwenye vita iitwayo Franco-Dahomenian war ambapo falme hii ilipoteza ushindi kwa mfaransa na kuchukuliwa kama koloni la ufaransa. Baadae ilikuja kupata uhuru mwaka 1958 ikajiita Republic of Dahomey….mwaka 1975 ilijibadirisha jina na kujiita Benin.

View attachment 2600605
[The real Agojie from Benin]

Mwaka 2015 Producer wa muvi za Hollywood Maria Bello alitembelea nchi ya Benin akakuta simulizi zinazowahusu hawa wanawake Agojie kwenye makumbusho akatamani sana stori hizo zitengenezewe muvi. Akarudi kwenye los angels akaanza kutafuta studio ambazo zitasapoti kutengeneza muvi kuhusu wanawake hao…studio ya STX ilitaka kutoa million 6 kama bajet ya muvi ila akakataa kwa kuona bajeti ndogo akapeleka idea yake kwenye studio zingine ila wakakataa kudhamini kutengeneza muvi hiyo.

View attachment 2600617

Mwaka 2018 ilipotoka muvi ya Black Panther ikapata mafanikio makubwa kifedha ukizingatia zilikua ni stori za kubuni tu, Maria akapata moyo wa kuendelea kutafuta studio itakayodhamini ndipo kampuni ya Tristar zikapata moyo na kudhamini muvi itengenezwe……Rupita Nyong’o na Viola Davis ndio walitakiwa wawe masterling wa muvi lakini Lupita akatolewa na kuwekwa pisikali Thuso Mbedu.

November 2021 wakaelekea south Africa kwa ajili ya kushoot kwa miezi mitano, asilimia kubwa ya Crew ilikua na wanawake Zaidi maana walitaka muvi iwe kiFeminine Zaidi ukizingatia Producer Maria Bello ni Lesbian wa muda mrefu, Hatimae muvi ikatoka September 2022 ikapwa jina la THE WOMAN KING.

View attachment 2600606


Wakati Stan Lee anatengeneza jeshi la wanawake watupu wa Dora Milaje kutoka kwenye comics za Plack Panther aliwatengeneza Dora milaje kutokana na simulizi za jeshi la wanawake watupu la agojie kutoka Benin…Ila akawafanya Dora milaje wawe wanafanana na wamasai maana Wakanda ni nchi iliyopo Afrika Mashariki. Ndio maana kama umetazama muvi ya Black Panther 1&2 utaona kua jeshi la Dora milaje wanavaa kama wamaasai.

View attachment 2600608
[Maasai Women from Tanzania]

View attachment 2600612
View attachment 2600614
[Dora Milaje Warriors from Black Panther]

Da’Vinci
Unenifanya ss nitafute hizi movie 2 niziwatch
Asante Kwa info
 
Done
Ss ngoja nimalizie na Wonder women
Jana nilianza woman king, very nice.

Nyingine nzuri tafadhali Ili ni watch pia
Pitia hapa bibie
 
Pitia hapa bibie
Asante
 
Eti Moderator wa mchongo [emoji23][emoji23][emoji23]
Wanazingua sana hawa watu..sijui kwanini wameleta hii mada Celebrity forum.

Ps. For you Tayana
 
Uzi mzuri sana Sir👏 .

Something new kutoka kwako naona umezingatia sana "Gender Balance" kama dunia ya leo inavyotaka.
Umenifurahisha sana ulivyoflow na Trend coz "Trend is a Friend", kwanzia kwenye past days, gender equality hadi kwenye current movies.

Best wishes Sir🙏
 
Wanazingua sana hawa watu..sijui kwanini wameleta hii mada Celebrity forum.

Ps. For you Tayana
Okay
Uko sahihi
 
Mkuu vipi kule alipotokea America Chaves kwenye Dr Strange 3, kuna wanaume?
 
Back
Top Bottom