Unawakumbuka Ma-Food Members?

Unawakumbuka Ma-Food Members?

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
Salam wakuu,

Hivi mnawakumbuka hawa jamaa? Hawakuna watu walikua wanajifanya wajuaji muda wa msosi shuleni kama mafud memba. Yaan hata kama darasani hamna kitu ila ukifika muda wa tea au msosi, hapo ndio utaona misifa ya hawa jamaa. Ukute sasa ni Co-school, hawa jamaa anaweza kukuchukulia hata demu wako na huto amini. Maana anaweza kumteka kwa vitu vidogo kama kuamrisha mpishi amuongezee nyama nk.

Usiombe iwe siku ya cha mzaramo aisee. Hapo unaweza ukatamani hata kumtukana mtu. Kuna food member wetu mmoja siku hiyo nimefika mbele kabisa ya mstari, simu imeita napokea anadai sina nifahamu nirudi nyuma kabisa ya mstari. Kilichotokea aisee, nilikula suspaa ya wiki mbili ila niliporudi tuliheshimiana.

Popote pale ulipo bwana Tingai, nakusalimu KWA jina la Jamhuri.
 
Mkuu umesomea st marrys nilifikiri unaongelea zile Shule zetu ugali wa dona umeiva kwa layers halafu maharage mixa mafuta ya taa unakula na wadudu wake ndani. Ugali kisado na maharage jagi na hushibi!
 
Mkuu umesomea st marrys nilifikiri unaongelea zile Shule zetu ugali wa dona umeiva kwa layers halafu maharage mixa mafuta ya taa unakula na wadudu wake ndani. Ugali kisado na maharage jagi na hushibi!
Mweh! Top layer naifahamu mkuu
 
Mweh! Top layer naifahamu mkuu
😂😂😂Top layer daah umenkumbsha mbali sana anyway nakumbuka mafud Lida wetu walikuwa na mtindo siku ya wali ndo wanagawa wao siku ya ugali wanakwepa kazi alaf hyo siku ya wali mfn jpl anajiwekea wapi mwingi anakula mpaka kesho yake mchana maan ilikuwa hawek mboga alaf pia MKOA tuliopo barid so chakula hakiharibik nakmbk walikuwa wanapenda kuweka wali wao Kwny mlango wa sufulia la kupikia 1day tulivunja kuful tikapita nao wali wao dadeq wajinga walilaan kama wameibiwa hela vile
 
Back
Top Bottom