Unawakumbuka waandishi gani na vitabu vyao waliovuma Sana hapa Tanzania?

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Kama umesahau Basi nakukumbusha wachache.

Alistabrus Elvis Musiba - Kufa na kupona, Njama, Kikomo

Faraj Hassan Hussein Katarambula - Simu ya Kifo, Pili Pilipili.

Hawa waandishi vitabu vyao vilitingisha Sana East Afrika.

Musiba alikua na Mhusika katika vitabu vyake aliekua Jasusi Mbobevu Afrika nzima Aliejulikana Kama Willy Gamba.

Unaweza kuongea idadi.
 
Prof. Amandina Lihamba - PENZI KITOVU CHA UZEMBE. Kilinifurahisha sana kile kitabu.
 
Kitabu kiliitwa Bado Mmoja kiliandikwa na Nikolas Marcus Kuzenza Sayuki.

Mwandishi mwingine aliiywa Hamie Rajab sikubuki vitabu vyake.
 
Watoto wa mama nitilie Semzaba
Jamaa alikiandika kikaandikika asee anyway
Kingine ni kwaheri ukoloni kwaheri uhuru .
Anyway kingine hiki hapa ila sio cha tz[emoji116][emoji116]
 
WALIOVUMA? Sema WANAOVUMA. Kuna Mkama, na Ali, na Mangula, na Ng'wanang'walu, na Kimario, na Alnoor Kassum , na mimi. Kama huwajui tuwasiliane upenu, unless you were jesting.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…