Bado sijaelewa nini unamaanisha,Disney ni studio inayojihusisha na utengenezaji movie.
Netflix ni website ya kupakulia movie au kuangalia mtandaoni,sindhani kama wanamiliki na studio ya utengenezaji movie.
Kwa maana hiyo hapo juu hao wawili hawawezi kushindana kwakuwa mmoja wao ni mkulima amabaye ni Disney na Netflix ni mchuuzi Wa mtandaoni.
Pia Netflix anakuwa akishirikiana na wakulima wengine ambao ni kama dream work na hawa nao pia wanazalisha bidhaa sawa na Disney wote wana tengeneza Animation
Ingekuwa poa kama unge washindanisha hao Disney na Dream work.
Na mwisho kabisa kuna Uzi upo Wa kulinganisha kazi za Sanaa ya katuni na zimetajwa studio nyingi jaribu kuutafuta utapata kujuwa ni Studio ipi ipo vizuri katika uzalishaji Wa katuni.