Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya kidato cha sita 2025, wanafunzi wamepokea taarifa hizo kwa hisia tofauti. Wapo waliopata matokeo mazuri, yakawapa nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu, jambo ambalo limeleta furaha na matumaini mapya katika maisha yao ya kielimu.
Hata hivyo, wapo pia wanafunzi ambao matokeo yao hayakufikia viwango vya kujiunga na vyuo vikuu. Kwao, huu unaweza kuwa wakati mgumu, wa masikitiko na maswali mengi kuhusu hatma ya maisha yao.
Ni muhimu kufahamu kwamba, hata kama matokeo hayakuwa mazuri kama ulivyotarajia, hiyo haimaanishi kuwa maisha yamesimama au kwamba umefeli milele. Hili ni jambo la muda na bado una nafasi kubwa ya kusimama tena, kupanga upya, na kuendelea na safari yako ya maisha kwa njia tofauti lakini yenye mafanikio.
MwanaJF, unawashauri nini wanafunzi