JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Hii ni kwa sababu Katiba ya JMT inampa haki mtu yeyote anapohisi au kuona haki yake ya Kibinadamu imeathiriwa na mtu mwingine au chombo chochote au Sheria yoyote, anaweza kufungua shtaka au lalamiko kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uwepo wa Sheria hiyo.
Wapo watu binafsi walioweza kufungua Mashtaka Katika Mahakama kuu dhidi ya Serikali kupinga Sheria zinazovunja haki za binadamu.
Christopher Mtikila mwaka 1993 alifungua shtaka akipinga Sheria ya Uchaguzi inayozuia mgombea binafsi asigombee katika uchaguzi mkuu.
Mtikila alishinda kesi na Mahakama ilisema kuwa Sheria ya Uchaguzi ipo kinyume na haki za binadamu ya kugombea nafasi za kisiasa.
Watu wengine pia wamewahi kufungua kesi kama Tito Magoti mwaka 2020 alipinga kifungu cha 148(5) ya Sheria ya mienendo ya Makosa ya Jinai inayozuia mtu kupata dhamana.
Na Rebecca Gyumi alipinga Sheria ya Ndoa inayoruhusu wasichana kuolewa wakiwa chini ya miaka 18.
Upvote
0