Unaweza kuokoa Pesa kwa kutumia Mtandao, ni basi tu hamtaki Kujiongeza!

Unaweza kuokoa Pesa kwa kutumia Mtandao, ni basi tu hamtaki Kujiongeza!

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Je, unajua kwamba bei za huduma nyingi za mtandaoni kama YouTube Premium, Netflix, Spotify, na hata tiketi za ndege au hoteli hubadilika kulingana na nchi uliyopo?

Kampuni nyingi hutumia bei tofauti kulingana na watu fulani, hii mbinu maarufu ya kibiashara inaitwa price segmentation na hufanyika ili kufikia watu kutonakana na uchumi wao. Hivyo mtu wa eneo moja anaweza kulipa bei tofauti na mtu wa eneo lingine. Watu wamekuja na mbinu za kufuata hizi bei nafuu hata kotoka nchi ambazo hawaishi, mbinu hii inaitwa “VPN exploit”. Sasa, kwa kutumia VPN (Virtual Private Network), unaweza kubadilisha IP yako na kuonekana kama uko nchi nyingine na ukanufaika na bei nafuu za nchi hiyo.

Your IP, your rules,. don't let them overcharge you..jpeg

Kwa mfano:
• Weka VPN yako ioneshe upo Nigeria au Argentina ili upate YouTube Premium kwa punguzo la bei na ukoe hadi 90% ya pesa yako ikilinganishwa na nchi za Magharibi.
• Kwa Netflix, jaribu Pakistan au Turkey utapa punguzo la bei hadi la 80%.
• Spotify inaweza kuwa nafuu zaidi kwa 85% ukiweka VPN yako ioneshe upo Turkey au India.
• Tiketi za ndege au hoteli zinaweza kuwa nafuu kati ya 20-40% ukitafuta wakati VPN yako inaonesha upo nchi kama Malaysia au Argentina.

Dunia ya sasa utalipa kulingana na ulivyokuja, ila ukiichukulia teknolojia serious, unaweza ukaokoa gharama nyingi sana za maisha kwa kufuata vitonga huko huko vinapopatikana na wala hauhitaji Passport kufanya hivyo, watu wanasema “Your IP, your rules” usikubali kampuni zikutoboe mfuko kwa bei za juu! Tumia VPN ili ujipangie bei unayoitaka.

Hii ni halali, lakini angalia mashart ya huduma husika. Jaribu VPN kama NordVPN au Surfshark, pia kuna hii VPN inaitwa Cyber Ghost ni nzuri sana katika harakati zako za kutafuta bei vitonga.

Binafsi natumia 1.1.1.1 ya CloudFlare ni mtelezo tu wa Vitonga vya Xbox game Pass nikitokea Bondeni kwa Madiba wakati kiuhalisia nimetulia zangu hapa downtown DSM.
 
Upo bongo unakata tiketi ikionesha upo turkey naomba kuuliza maswala ya ku seti destination Yako unafanyaje huku safari Yako ni ya kuanzia KIA to Amsterdam kwa mfano? Au sijaelewa vizuri?
Hata Mimi sijamuelewa vizuri
 
Upo bongo unakata tiketi ikionesha upo turkey naomba kuuliza maswala ya ku seti destination Yako unafanyaje huku safari Yako ni ya kuanzia KIA to Amsterdam kwa mfano? Au sijaelewa vizuri?
Okay… haijalishi upo wapi… kwenye usafiri wa anga haimaanishi mtu anavyokata tiketi akiwa Singapore kuelekea Marekani basi atakuwa kweli yupo Singapore.. Watu wanaosafiri sana huwa wanajua kama atakuwa sehemu fulani siku fulani. Mfano nikikataka Ticket ya ATCL Kutoka Dar kuelekea Mwanza haimaanishi huo muda nipo Dar, inawezekana nipo Morogoro ila nitakuwa Dar hiyo siku ya Safari.

Ticketing portal huwa zinatoa offer kulingana na mahali mtu alipo, kwa kesi hii naweza nikawa nipo Kenya naelekea Uengireza, lakini nikabook wakati VPN inaonesha nipo India ni wazi nitapata offer za geographic hiyo kwa kuestimate uchumi wangu huku kampuni ya ndege wakijua huyu mtu kwa sasa yupo india ila atakuwa Nairobi Kenya kwa shughuri nyingine hiyo siku safari.
Na hapa unaweza ukapata unafuu si tu kwakuwa ulibook kutokea India lakini pia punguzo kwakuwa ulibook in advance
 
Upo bongo unakata tiketi ikionesha upo turkey naomba kuuliza maswala ya ku seti destination Yako unafanyaje huku safari Yako ni ya kuanzia KIA to Amsterdam kwa mfano? Au sijaelewa vizuri?
Hata Mimi sijamuelewa vizuri
Inawezekana, unakata tiketi ya kwenda popote, kutokea popote na ukiwa popote,
Mfano origin ni kia, destination ni Amsterdam na wewe inaonesha upo China labda, hakuna tatizo muhimu ni jina la kwenye ticket na passport vilingane na uwepo wakati wa kusafiri kwani inawezekana kumtumia mtu mwingine akukatie ticket mfano travel agents au airline company
 
Nimeelewa kwa upana zaidi. Weka link ya 1.1.1.
 
Hata Mimi sijamuelewa vizuri
Hipo hivi uzwaji wa tiketi za ndege hakuna restriction.Mtu anaweza kuwa ulaya haka kukatia teketi kwao na kutumia namba kama una passport.

Hapa uwanja wa ndege juliasi unaweza kwenda na Number ya tiketi ambayo itaonesha jina lilopo kwenye passport au kitambulisho ukapewa tiketi ya karatasi hapo hapo.
 
Back
Top Bottom