Je, unajua kwamba bei za huduma nyingi za mtandaoni kama
YouTube Premium,
Netflix,
Spotify, na hata
tiketi za ndege au hoteli
hubadilika kulingana na nchi uliyopo?
Kampuni nyingi hutumia bei tofauti kulingana na watu fulani, hii mbinu maarufu ya kibiashara inaitwa
price segmentation na hufanyika ili kufikia watu kutonakana na uchumi wao. Hivyo mtu wa eneo moja anaweza kulipa bei tofauti na mtu wa eneo lingine. Watu wamekuja na mbinu za kufuata hizi bei nafuu hata kotoka nchi ambazo hawaishi, mbinu hii inaitwa “
VPN exploit”. Sasa, kwa kutumia
VPN (Virtual Private Network),
unaweza kubadilisha IP yako na kuonekana kama uko nchi nyingine na ukanufaika na bei nafuu za nchi hiyo.
Kwa mfano:
• Weka VPN yako ioneshe upo
Nigeria au
Argentina ili upate
YouTube Premium kwa punguzo la bei na
ukoe hadi 90% ya pesa yako ikilinganishwa na nchi za Magharibi.
• Kwa
Netflix, jaribu
Pakistan au
Turkey utapa punguzo la bei hadi la 80%.
•
Spotify inaweza kuwa
nafuu zaidi kwa 85% ukiweka VPN yako ioneshe upo
Turkey au
India.
• Tiketi za ndege au hoteli zinaweza kuwa nafuu kati ya
20-40% ukitafuta wakati VPN yako inaonesha upo nchi kama
Malaysia au
Argentina.
Dunia ya sasa utalipa kulingana na ulivyokuja, ila ukiichukulia teknolojia serious, unaweza ukaokoa gharama nyingi sana za maisha kwa kufuata vitonga huko huko vinapopatikana na wala hauhitaji Passport kufanya hivyo, watu wanasema “Your IP, your rules” usikubali kampuni zikutoboe mfuko kwa bei za juu! Tumia VPN ili ujipangie bei unayoitaka.
Hii ni halali, lakini angalia mashart ya huduma husika. Jaribu VPN kama
NordVPN au
Surfshark, pia kuna hii VPN inaitwa
Cyber Ghost ni nzuri sana katika harakati zako za kutafuta bei vitonga.
Binafsi natumia
1.1.1.1 ya CloudFlare ni mtelezo tu wa Vitonga vya
Xbox game Pass nikitokea Bondeni kwa Madiba wakati kiuhalisia nimetulia zangu hapa downtown DSM.