Watu wengi wenye sifa duniani hawajawahi kupata mapenzi ya kudumu. Kesi yako inaweza kuwa tofauti.
Inaonekana kwamba ndani yetu kuna nafasi kubwa ambayo haiwezi kujazwa na wachumba mia. Hata hivyo kuna tumaini. Ndoto lako linaweza kutimizwa.
Thubutu kufikiri
Mwanamke anafaa kupendeza kiwango gani kumfanya asitake upendo tena? Mwanaume anahitaji kuona vipusa wangapi uchi kabla ya kujisikia kama anapendwa? Kila kitu ndani yetu inalilia upendo! Sote tunatafuta upendo, hakuna kitu kinachoweza kuchukua nafasi ya upendo. Wanasayansi na madaktari wamethibitisha kwamba watu wanaofuata umalaya, na aina za ngono zisizo kawaida huwa wanatafuta upendo wa kweli.
Hata hivyo kupata upendo ni jambo tata. Sura mzuri hunyauka. Mchumba hugeuka. Ndoa inaweza kuvunjika mkeo/mumeo akifa. Na uchungu utakayo hisi huzidi kama upendo kati yenyu ni kubwa zaidi.
Ukweli kwa wengi hutisha sana, lakini matarajio yetu huwa hazishikiki! Matakwa yetu ya ndani kabisa huonekana kuwa mbali sana hadi sisi hujaribu kuvikana. Kana usikane, kubali ukatae matarajio yetu hubaki ndani yetu.
Kwa muda mfupi tu, hebu tazama matarajio yako...usijali ugumu wa kuzipokea. Angalia matarijio yako, ona kile zinakuambia.
Unamtaka mtu ambaye:
* atafanya usikie kama umeheshimika
* anakuamini na unamuamini
* hamna siri kati yenyu
Kwa ndani unatamani mtu mwenye:
* werevu, nguvu, uzuri usionyauka hata akizeeka
* anajua yote ambayo umepitia maishani na hata alikuwa na wewe
* atakuelewa kabisa kila wakati
Unamtaka mpenzi yule:
* atatimiza mahitaji yako kikamili, yani ni kama mliumbwa muwe pamoja
* anasikia uchungu na wewe na anweza kukusaidia hata kuharibike vipi
* anajuauovu wako, fikira zako na bado anakupenda na anakuheshimu
* anaweza kuwa na wewe mahali popote wakati unamhitaji
* atakupenda daima na mapenzi kuu yenye kukufurahisha na kukutosheleza
* anakusaidia kila wakati na kukuwezesha kufanya makuu
Unahitaji mtu atakaye kusaidia kila wakati, lakini anakupatia nafasi ya kukuwa kibinafsi; mtu ambaye hatakuchosha, na ambaye hatawahi kugueka.
Mwishowe, liwe liwalo, unataka kuwa huru kutokana na uwoga wa kumpoteza mpenzi wako. Unataka mpenzi ambaye hata wahi kugonjeka, kulemaa au kufa.
Ninayosema inaonekana kama upumbavu!