Michezo ya video 'video game' ina faida kimwili, kisaikolojia, na kijamii. Kutokana na namna michezo hiyo huhusisha akili, ambayo inaweza kumsaidia mtu kukuza uwezo wake wa kuchanganua mambo.
Michezo hii inaweza kusaidia wale wanaosumbuliwa na uraibu au hamu ya kupunguza nguvu za tamaa za vitu vyenye madhara, kama madawa ya kulevya na pombe. Inasaidia pia kuchangamsha ubongo na kuufanya uwe na uwezo mkubwa kiutendaji. Inashauriwa pia kucheza michezo hii kwa kiasi, ili kuepusha uraibu na kupata muda kupumzisha akili.
View attachment 1746611