Unaweza kurudia darasa la saba endapo ukifeli kwa miaka hii?

GOSSO MZEKEZEKE

Senior Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
180
Reaction score
204
Habari wana JF

Kuna mtoto wa dada yangu anauwezo mkubwa sana ila amesoma katika mazingira magumu sana ya kijijini lakini hajafanikiwa kufaulu vizuri.

Huku tukiendelea kusubiri selection nafikiria nimchukue aje arudie darasa la saba huku mjini ili aendelee na secondari.

Lakini kutokana na mazingira ya technolojia na majibu kutoka mtandaoni, Je anaweza kurudia darasa la saba tena au anafanyaje ili apate shule ya serikali mwakani endapo mwaka huu akikosa?

Amepata grade C. Naombeni mwenye uelewa anijuze namna ya kumsaidia.

NB; Uwezo wa kumsomesha private sina.
 
Nimesikia kuna utaratibu saiv wa kurudia darasa la 7 kwa waliofeli, kuna form zipo zinatolewa (sema utaratibu wake sijaufatilia) na anarudia kwa jina lake hilo hilo bila kubadili.

Ukiona vipi ndy umpeleke shule nyingn ama hiyohiyo aliyosomea kwa jina lingine tena. Upo utaratibu wa kufuata, ukifuatilia utajulishwa.
 
C amefaulu, atachaguliwa shule ya serikali.

Akiwa f1 hakikisha anahudhuria siku zote 194 hata kama anaumwa malaria, awe na sare safi, madafutari ya kutosha na uwe unajenga mawasiliano ya karibu kati yako na mwl wa darasa, nidham na taaluma. Pia usisahau kuwatoa walimu wake buku 5 au muda wa chai unawatoa chapati mbili kila mtu.

Mpwa wako atahudumiwa kama mla tozo na vitabu vyote atapewa bila kuandikwa popopte.

Msisitze awe na nidham
 
Nashukuru nitafuatilia
 
Sawa, nitalifanyia kazi hilo
 
Back
Top Bottom