youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,811
- 3,888
Unaweza kusajili leseni ya biashara kwa kutumia cheti cha jina la biashara yako tu
Leseni ya biashara ni kibali rasmi kinachotolewa na mamlaka husika ili kukuruhusu kufanya biashara kwa mujibu wa sheria. Bila leseni, biashara yako haina utambulisho wa kisheria, jambo linaloweza kukukosesha fursa nyingi muhimu.
Aina za Leseni za Biashara
- Leseni ya biashara Kundi “A”
- Leseni ya biashara Kundi “B”
Vigezo vya Kuomba Leseni kwa Kutumia Jina la Biashara
Ili kusajili leseni kwa jina la biashara yako, unachohitaji ni:- Cheti cha usajili wa jina la biashara
- Taarifa kutoka kwa msajili (Extract from Register) kwa majina ya biashara pekee
- Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ya mwenye biashara
- Tax Clearance Certificate (kwa anayehuisha leseni)
- Uthibitisho wa sehemu ya kufanyia biashara (mfano mkataba wa pango, hati ya umiliki au leseni ya makazi)
- Uthibitisho wa uraia na ukaazi
Faida za Kuwa na Leseni ya Biashara
Kusajili leseni ni uwekezaji katika biashara yako. Faida zake ni nyingi, Mfano:- Kufanya biashara yako kutambulika kisheria
- Kuaminika na taasisi za kifedha kama benki (kwa ajili ya kufungua akaunti)
- Kupata nafasi ya kuomba mikopo ya kibenki na ya kifedha
- Kuongeza fursa za zabuni na kazi mbalimbali
- Kujenga uaminifu wa wateja, kwasababu biashara yenye leseni huonekana halali na thabiti
Utaratibu wa Kupata Matokeo ya Ombi
Mara baada ya kukamilisha maombi yako, utapokea taarifa kupitia email na namba ya simu uliyoandika kwenye mfumo. Ujumbe huu utakujulisha matokeo ya ombi lako, na unaweza kuyaona sehemu ya “print-outs” ndani ya akaunti yako.- Ikiwa ombi lako lina mapungufu, utapokea maelekezo ya kurekebisha kupitia barua pepe. Ukisharekebisha, utalirudisha tena BRELA kwa ajili ya kushughulikiwa.
Njia rahisi sana ya kupata leseni ya biashara yako
Ikiwa unahitaji leseni, kufungua kampuni au hata kusajili jina la biashara, tunakusaidia kukamilisha hatua zote haraka na kwa uhakika.Fika ofisini kwetu au wasiliana nasi kwa simu +255693880325. Pia, tunatoa huduma online popote ulipo ndani ya Tanzania, tunakuhudumia bila wasiwasi.