Unaweza kutembelea Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani

Unaweza kutembelea Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani

Joined
Jul 6, 2023
Posts
40
Reaction score
83
Baada ya pilika pilika za mwezi mzima, siku moja unaweza kupanga kutembelea Wilaya ya Mkurunga Mkoani Pwani na kugundua ziwa moja wapo linalopatikana mkoani hapa.

Hili ni ziwa Mansi, linapatikana takribani kilomita 70 kutoka Dar es Salaam. Sio mbali sana na jiji la Dar es salaam na kama hukuwahi kupita njia ielekeayo kusini mwa Tanzania basi utafurahia kuona idadi kubwa ya miti ya minazi njiani na barabara nyembamba na mfululizo wa majengo ya viwanda mbali mbali kote njiani.

Ukiwa unaelekea huko, kama utatumia usafili wa uma, utapaswa kushukia eneo linaloitwa Mwarusembe, ni rahisi zaidi kulifikia ziwa hilo kama utaanzia kutembea kutokea hapo. Kwa ushauri zaidi kama utaenda kwa shughuli za kitalii ni bora kutembea kwa miguu kutokea hapo Mwarusembe hadi ziwani. Kwanini nashauri hivyo? Ukiwa njiani utaweza kupata fursa ya kuona aina ya nyumba za nyasi zitumikazo kama makazi na utamaduni wa watu wa kabila la wazaramu, kuwa kama sehemu ya mazoezi na kupata utulivu kukatisha katika maeneo tulivu usiyoyazoea.

Binafsi nilijaribu jambo hili na nikiwa njiani nilibahatika kuona mambo mengi na kupata utulivu wa nafsi kutokana na ukimya na utulivu mkuu kote njiani.

Na kama pia unatumia usafiri binafsi unaweza kuchepusha maeneo hayo na kupata uelekeo kirahisi kusogea kukaribia eneo lilipo ziwa Mansi. Ni rahisi kufika huko, lakini kumbuka kusema nataka kufika bwawani, kwa kuwa wenyeji wengi huko hawafahamu kama hilo ni ziwa.

Nini utegemee kukutana nacho? Hapo ndio kwenye kazi sasa. Hili ni ziwa lenye kuzungukwa kwa kiasi kikubwa na uoto asili na mazao ya kupandwa. Kwa sehemu kubwa limegawanyika kwa maeneo yenye maji na maeneo mengi yenye magugu na uoto mwingi.

Huko uvuvi wa kienyeji ufanyika, wavuvi wengi wazawa wa maeneo hayo hujipatia kipato kwa kuvua samaki wanaopatikana ndani ya ziwa hilo. Hivyo ni rahisi kwako kuweza kupata wasaa wa kupanda mtumbwi na kuona mandhali ya ziwa mansi kupitia wenyeji wanaopatikana huko.

Usitegemee kukutana na wageni wengi au watu wengi wanaoenda kutembelea huko, lakini utaweza kuona jambo jipya na kujifunza kitu kipya juu ya uwepo wa ziwa hili katika wilaya hii kubwa ya Mkuranga.

Karibu mkoa wa Pwani karibu kutembelea ziwa Mansi.

#All about Tanzania life 🔴🟠⚪️

1720043764279.jpg
 
Nikipata nafasi nitaenda ila...

Wenyeji wanajua na kuliita bwawa wewe mgeni wa muda mfupi unatuambia ziwa, sasa nani anajua zaidi kati yako na wenyeji walioliona bwawa likiwa kijito kidogo hadi sasa baada ya uharibifu wa mazingira over climate change na kuwepo bwawa hilo?.
 
Nikipata nafasi nitaenda ila...

Wenyeji wanajua na kuliita bwawa wewe mgeni wa muda mfupi unatuambia ziwa, sasa nani anajua zaidi kati yako na wenyeji walioliona bwawa likiwa kijito kidogo hadi sasa baada ya uharibifu wa mazingira over climate change na kuwepo bwawa hilo?.
Hii ni kutokana na mazoea ya watu. Binafsi nililiona ziwa hili kupitia Google map, na siku nilipotembelea huko ndipo nilipogundua kuwa wenyeji wanalitambua kwa jina la Bwawa. Niliulizia uelekeo wa Ziwa Mansi kwa zaidi ya watu wa tano lakini, hawakuwa wanalijua. Mwishoni ndipo nikataarifiwa kuwa kuna bwawa Mansi labda niende huko.
 
Hii ni kutokana na mazoea ya watu. Binafsi nililiona ziwa hili kupitia Google map, na siku nilipotembelea huko ndipo nilipogundua kuwa wenyeji wanalitambua kwa jina la Bwawa. Niliulizia uelekeo wa Ziwa Mansi kwa zaidi ya watu wa tano lakini, hawakuwa wanalijua. Mwishoni ndipo nikataarifiwa kuwa kuna bwawa Mansi labda niende huko.
Hivi wenyeji na google nani wa kwanza kuwepo eneo husika?.

Ni sawa kwa wasukuma, wajita na wahaya 'old age' uwaambie khs ziwa nyanza ambalo mmekuja kuliita Victoria, je wao hawakuwa wanaliona na kutumia maji yake?.

Ila alipofika sijui mgundizi wenu akasema kagundua ziwa, ah🤔!.
 
Sema watu wa mkuranga ni noma sana hawakai na kitu rohoni kule ni kawaida kabisa ukifika tu hata kama hawakujui mtu kukueleza mambo yake yòooote mpaka unashangaaa
Nilienda mkuranga nikiwa kwenye gari konda anaongea huyo mambo ambayo hapaswi kuongea public, nilivyoshuka nikachukua boda, yule boda njiani ananiambia mambo yake mimi hata simsikii vizuri kwa ajili ya upepo nikabaki kushangaa tu huyu mtu vipi hatujuani lakini ananieleza maisha yake na sijamuuliza, kumbe ndio tabia zao.
 
Back
Top Bottom