Unaweza kutembelea Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani

Mkuranga au mkurunga mi nilifikiri ni mahali kwingine.
Anyway sio ziwa ni bwawa.
Nilipita rouge road kuelekea masaki kuna mlima huko kati niliona hilo bwawa kwa chini
 
Ndio walivyo wote mkuu kama una jamaa yako mtu wa Mkuranga angalia vya kumwambia siku ya kwanza naenda kununua kiwanja,

Nikakutana na mzee muuzaji alinipa habari mpaka za wajukuu zake nikawa najua mjuu wake wa Tanga kaachwa, mwanae wa kiume kazamia kwa kaburu, mkwe wake kawa teja na mambo mengine mengine mengi tu naenda kwa mtendaji huko ndo balaa ananipa stori kuhusu tabia ya mkewe kuunguza samaki na kashamkanya sana

Sijakaa sawa anaingia mgambo wa kijiji akanipa habari nyumbani kwake kuna mchawi🤣🤣🤣
 
Nmetamani sana kupata shamba mkuranga ila mwenyeji wangu anataka kuhama kumuuliza sababu nini anadai wanga sana😂
 
Ah ah na wewe ungewapa intro kidogo 😁😁
 
Umesahau au hujaambiwa kuna chatu wakubwa ambao wanaweza kumeza mtu mzima mzima.

Inatakiwa kuwa makini na nyoka pia ni wengi.

Huko ni kuzuri sana kwa mtu anaetaka kuwekeza kwenye mazao ya nyoka.
 
Ni sehemu nzuri kupata utulivu wa nafsi na kugundua eneo jipya la kujiwekea kumbukumbu zako binafsi. Karibu sana mkuu.
Mkuu bila kusahau ziwa Zakwati lililopo Mkola namna ya kulifikia kwa usafiri wa binafsi kwa njia ya kusini unaipita Kimanzichana na Mkiu unakwenda mbele unakuta kiwanda cha vioo unaendelea mbele si mbali sana unakuta kiwanda cha tailizi cha Goodwill unakipita kwa mbele kidogo unakuta kijiji cha Nyamalonda hapo unaingia kushoto njia ya kwenda Magawa una kwenda hadi Lukanga hapo unaachana na njia ya Magawa una kata kushoto hadi Mkola unakuwa umefika ziwa Zakwati.
 
Kwa muonekano hilo ni ziwa kabisa. Kuanzia ekari tano hilo ni ziwa. Vipi kuhusu mamba na viboko, wapo humo?
 
😂 kwao hawahitaji kulewa ili kumwaga siri za watu, watoto wakizaliwa maeneo yao kiasili si wanabeba izo tabia pia?

Niliambiwa huko mabinti wadogo sana wanaolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…