Unaweza kutoa pesa ili kupata ajira? Ni vipi utahakikisha kuwa hautapeliwi?

Unaweza kutoa pesa ili kupata ajira? Ni vipi utahakikisha kuwa hautapeliwi?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Nakumbuka nilishawai kuitwa sehemu kufanya internship kwa ahadi nikimaliza internship nitapata ajira.

Ila baada ya HR kivuli kustukia mchongo likaanza zwenge la kunishinikiza nitoe pesa ili nipewe kazi binafsi sio muumini wa rushwa; nilikataa hapo ukaanza mvutano kati ya head of department na HR baadaye nikaona isiwe kesi nikawaaga tu.

Huku nyuma jamaa wakanifuata wakanambia mpe hela mmalizane na HR mbona hata sisi tumeingia na hela wewe vipi. Nikawajibu siwezi kufanya ujinga huo, elimu ninunue mpaka kazi nayo ninunue? Basi wakaniona boya sana.

Swali, je unaweza toa pesa ili upate ajira na unahakikisha vipi kwamba hautatapeliwa?
 
Kutoa na kupokea rushwa ni kosa kisheria. Tafadhari ripoti Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU
 
Vyeti tupu vilivyopendeza ukiviweka kwenye frem ukavitundika ukutani ukawa unaviangali unaweza ukala ugali bila mboga au ukaenda kukopea mkopo bank[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Basi endelea kutazama vyeti huku huna hata kibarua cha kujitolea, ugali wa 'shkamoo mama' mtamu sana!

Usiku utapokwisha…[emoji276]
 
Nilifanya hivo mwaka 2019. Wiki moja baada ya form 6 nikiwa na girlfriend wangu tunazurula nikakutana na rafiki yangu aliyeacha shule form 2 akafurahi kuniona maana niliwahi mpigia interview kijanja kwa Wahindi akapata kibarua. Akanambia ameacha kazi kule anafanya kazi sehemu nyingine na kuna nafasi uko zipo anajua naweza bila hata training.

Nikakutana na HR na vyeti vyote ikahitajika laki nikajilipua nikaitoa. Mpaka nafikia muda wa kuja chuo nishachukua 1.1M, wale wazalendo waliokuwa JKT walikuja na matusi.
 
Back
Top Bottom