Unaweza kutumia chombo gani huru kuupata ukweli wa yasemwayo na Wanasiasa katika nchi yako?

Unaweza kutumia chombo gani huru kuupata ukweli wa yasemwayo na Wanasiasa katika nchi yako?

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,418
Reaction score
4,031
Raisi Donald Trump aliwahi kudai kaibiwa kura akiwa madarakani. Kura zikarudiwa kuhesabiwa baadhi ya majimbo( Georgia), matokeo ya pili yakaonyesha bado ameshindwa! Akakubali matokeo. Hii ina maana, kiongozi "Mkubwa" katika nchi anapoongea jambo inafaa kama lina ukakasi,kuwepo na chombo kingine cha kuclear doubt pale linapoonekana hasa kuathiri maslahi ya jamii fulani.

Nimefuatilia uchaguzi Mkuu unavyotakiwa kufanyika nchini Ghana, nikalinganisha na matamko ya wagombea uraisi,nimejidhisha. Kuwa kuna njia za wazi za kuclear doubts pale mmojawapo hataridhika,na wananchi wengi pande zote wako happy.

Jana nimesikia kauli mbili tofauti za Viongozi wakuu kule Zanzibar na waliokuwa wagombea wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Mmoja anamwapisha mwenzake awe msaidizi wake kwa mujibu wa katiba. Mwapishaji anaamini ndiye Mkuu wake halali na anasema nchi ni yetu sote tunapaswa kuitumikia bila mizozo. Anayeapishwa anasema kesi aliyofungua ICC iko palepale na imekuwa ngumu kwake kuamua kukubali uteuzi. Hii ina maana kuna jambo haliko sawa. Je, ni njia ipi na ya Kizalendo inayoweza kuuweka wazi ukweli wao?

Ni nini kinachosababisha kukosekana kwa vyombo huru kama ilivyo Marekani au Ghana kuchunguza na kubaini ukweli wa Viongozi wetu wa kisiasa?

Ninaamini wananchi tulio wengi tusingependa kuona viongozi wetu wakisigana na Chombo huru ndiyo mwarobaini wa ukweli.
 
Back
Top Bottom