Unaweza kuugua au kufa ukila maharagwe mekundu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1574850616224.png

Kwa ujumla huwa tunasema kuwa maharage ni mazuri kwa afya, lakini kuna aina ya maharage kama hayataandaliwa vizuri yanaweza kukufanya uugue ukila.

Maharage mekundu ndio aina ya maharage ambayo yanatajwa kuwa na ladha nzuri, yenye virutubishi, protini, vitamini na madini. Lakini kwa upande mwingine aina hiyohiyo ya maharage ina sehemu inayojulikana kama 'phytohaemagglutinin' ambayo huwa sio rahisi kuyeyuka.

Kama ukijaribu baada ya muda, jiandae kutapika na maumivu ya tumbo.

Habari njema ni kuwa kama maharage hayo yakipikwa vizuri , madhara kama hayo yanaweza yasikupate. Kama ilivyo kwenye maharage mekundu, maharage ya soya pia yana protini lakini ya sumu asili ambayo mtu unapaswa kuwa makini kuyaandaa.

Ni vyema maharage hayo yakalowekwa kwenye maji walau saa 12 kabla ya kuchemshwa.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hivi kuna maharage yanaweza kulika bila kuiva vizuri kweli....hizi tafiti nyingine kunyimana raha tu.
wameshauri yaweze kulowekwa kwa masaa 12, ni wengi hupata kiungulia na hamjui hizi kitu aisee tukubali ukweri
 
Maharage yana sumu ukila mabichi yakipikwa sumu inatoka hata miongo baadhi isipokuwa treated vizuri inaua, kwahio kila kitu kinahitaji preparation fulani ili kiweze kulika
 
Naona lengo la hawa mabeberu sasa ni kutaka tufe kwa njaa maana kila kitu kina sumu...
 
Kwa ujumla huwa tunasema kuwa maharage ni mazuri kwa afya, lakini kuna aina ya maharage kama hayataandaliwa vizuri yanaweza kukufanya uugue ukila.

Maharage mekundu ndio aina ya maharage ambayo yanatajwa kuwa na ladha nzuri, yenye virutubishi, protini, vitamini na madini. Lakini kwa upande mwingine aina hiyohiyo ya maharage ina sehemu inayojulikana kama 'phytohaemagglutinin' ambayo huwa sio rahisi kuyeyuka.

Kama ukijaribu baada ya muda, jiandae kutapika na maumivu ya tumbo.

Habari njema ni kuwa kama maharage hayo yakipikwa vizuri , madhara kama hayo yanaweza yasikupate. Kama ilivyo kwenye maharage mekundu, maharage ya soya pia yana protini lakini ya sumu asili ambayo mtu unapaswa kuwa makini kuyaandaa.

Ni vyema maharage hayo yakalowekwa kwenye maji walau saa 12 kabla ya kuchemshwa.

Chanzo: BBC Swahili
Maharage ya kiburu[emoji39]
 
Wananchi hawataki mchezo na mboga ya taifa

Naona mnagomea tafiti
 
Uku mbeya tumekula Sana naona wew nawe unatumiwa na mabeberu
 
Back
Top Bottom