Kubadilisha maisha mazima ni kuwa na ule msukumo wa ndani kabisa wa kufanya maamuzi kuliendea jambo fulani au kufanya jambo fulani
Watu wengi tunajua nini cha kufanya ili tubadili maisha yetu kutokana na tabia fukani fulani lakini hatuna msukumo wa ndani kufanya mabadiliko hayo
Mfano umesema unapenda fast food / madada poa lakini unajua kwamba huo sio muenendo mzuri na unataka kuachana nao,,,kwahiyo unachohitaji hapo ni nyenzo na msukumo toka ndani ya nafsi yako kuamua kuachana na tabia hiyo,,,hao walioweza hawakuwa na nguvu za ajabu zaidi ya kuamua kubadilisha mwenendo wa maisha yao,,hata wewe pia unaweza
Unajua nini mwamba? Tofauti ya waliofanikiwa kubadilisha maisha yao mazima ni MAAMUZI YA KUFANYA NA KUTOFANYA,,,,wao wameamua kufanya na wengine wameamua kutofanya na hiyo ndio tofauti
Mfano huyo rafiki yako amekwambia ana mtu wake toka shule ya msingi na ndio anataka kumuoa,,,yeye aliamua kuwa na mtu mmoja tu na akalisimamia hilo,,,tofauti na wewe ambaye uliamua kuwa na wachumba wengi wa fast food na ukalisimamia hilo,,,ishu hapo ni maamuzi ya dhati kuliendea jambo fulani
Haijalishi utapata falsafa ngapi au kufuata falsafa gani ila kama huna maamuzi ya dhati ambayo utayasimamia basi usitegemee maisha yatabadilika
Ni hayo tu!