Unawezaje kubadilisha maisha yako Daima??

Mtu kashuka vizuri na Uzi wake murua,alafu Kuna muhuni mmoja kwenye comment ya pili tu anakuja kuchanganya madawa na swali la kukata moto kabisa.

Eti "ushapona tatizo la kuwa na harufu Kali?"

Nimecheka sana asee!!
ndio walimwengu
 
Kubadilisha maisha mazima ni kuwa na ule msukumo wa ndani kabisa wa kufanya maamuzi kuliendea jambo fulani au kufanya jambo fulani

Watu wengi tunajua nini cha kufanya ili tubadili maisha yetu kutokana na tabia fukani fulani lakini hatuna msukumo wa ndani kufanya mabadiliko hayo

Mfano umesema unapenda fast food / madada poa lakini unajua kwamba huo sio muenendo mzuri na unataka kuachana nao,,,kwahiyo unachohitaji hapo ni nyenzo na msukumo toka ndani ya nafsi yako kuamua kuachana na tabia hiyo,,,hao walioweza hawakuwa na nguvu za ajabu zaidi ya kuamua kubadilisha mwenendo wa maisha yao,,hata wewe pia unaweza

Unajua nini mwamba? Tofauti ya waliofanikiwa kubadilisha maisha yao mazima ni MAAMUZI YA KUFANYA NA KUTOFANYA,,,,wao wameamua kufanya na wengine wameamua kutofanya na hiyo ndio tofauti

Mfano huyo rafiki yako amekwambia ana mtu wake toka shule ya msingi na ndio anataka kumuoa,,,yeye aliamua kuwa na mtu mmoja tu na akalisimamia hilo,,,tofauti na wewe ambaye uliamua kuwa na wachumba wengi wa fast food na ukalisimamia hilo,,,ishu hapo ni maamuzi ya dhati kuliendea jambo fulani

Haijalishi utapata falsafa ngapi au kufuata falsafa gani ila kama huna maamuzi ya dhati ambayo utayasimamia basi usitegemee maisha yatabadilika

Ni hayo tu!
 
Mkuu nimekuelewa
 
Ukiwa unatembea na Machangudoa, huwezi kukosa ka harufu fulani kanakokera. Kumbe jibu la suala lako ni hilo

Ref:
 
we n bikra hapo??
umetembea na watu wangap?
Changudoa n anaejiuza tofauti n kujiuza lakini mtu yule yule akigawa bure anaitwa malaya!!

So hao uliotembea nao unajua wamewapea watu wangap
 
Mimi nimekueleza chanzo cha harufu mbaya. Ukiacha kuhangaika na machangudoa harufu itakoma.
😅😅😅😂😂😂mkuu sina hilo tatizo si kila mada hapa ni zangu zingine napost kwa niaba
 
Nilikua chuo mwaka fulani na kulikua na shida ya usafiri wa magari yanayoenda chuo afu niparefu sana. Costa zinajaza watu wanasimama na ni umbali mrefu nilisimama mara kadhaa mpaka siku nikajisemea moyo

“Siwezi kabisa haya maisha, kusimama n mateso mi nataka kila nikisafiri nikae”

Basi nikajiwekea malengo Gari yyte itayoingia lazima niwai nipate siti hata kama Ataingia mtu mmoja huyo mmoja awe ni mimi”

Tangu siku hyo maisha yangu yalibadilika daima mpaka namaliza shule sikuwahi kusimama tena.

So huu ni mfano mdogo lakin impact yake ni kubwa.Hivo hivo kwene maisha unaweza kuweka maagano y kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…