Unawezaje kufanikiwa bila nguvu ya ziada nyuma yako?

Mkuu,mbona Ibrahim,Daud na Suleman walikuwa matajiri wakubwa na walimtegemea Mungu?
mwisho wa safari unajua nini kilitokea?suleman alikiri wazi huu ni upuuzi mtupu,wakati ayubu akinyang,anywa kila kitu na kupewa baadae.

halafu mkuu,unajua baada ya agano jipya nini kinaendelea!,zamani hata kuoa wake zaidi ya mmoja ilikuwa ni baraka kutoka kwa Mungu.
 
asante mkuu,wewe sio mlokole masuti.
 
Maombi hayawezi kukufanya utajirike bali unaomba Mungu akufungue akili zaidi. Swala la Kufanikiwa ni wewe na wewe. Mungu anakupa afya njema tu.
 
Maana ukishazaliwa na wazazi tu, tayari mtu mwingine kashachangia katika mafanikio yako kwa namna moja ama nyingine.


👆🏻 Sasa hao wazazi walikujaje hapa duniani kama siyo Mungu aliyewaleta (super natural being)

Popote ukimbiliapo huwezi kumkosa Mungu, Yeye ndiye "CAUSA CAUSANS", mwanzilishi wa kila kitu.
 
Mkuu elezea vizuri unajizaaje?
Sijaandika unaweza kujizaa, ningeandika hivyo, swali la unajizaaje lingekuwa sawa sawia kwangu.

Nimeandika unahitaji kujizaa.

Unaweza kuhitaji kurudi mwaka uliokuwa darasa la kwanza lakini usiweze.

Point yangu ni kwamba, hakuna mtu aliyefanikiwa bila kuhitaji msaada wa wengine, kwa sababu kwanza wote tunazaliwa na wengine.

Ili mtu aweze kusema kafanikiwa bila ya msaada wa wengine, itabidi maisha yake yaanze kwa kujizaa mwenyewe, kitu ambacho hakiwezekani kwa sexual reproduction yetu.
 
Point yangu ni kwamba, hakuna mtu aliyefanikiwa bila kuhitaji msaada wa wengine, kwa sababu kwanza wote tunazaliwa na wengine.


Kuzaliwa ndiyo aina moja ya kuumbwa, kwa sababu hatua zote hadi mtoto kuzaliwa hujiendesha (automatically), ni hatua moja tu ndio wazazi uhusika sana nayo ni tendo la ndoa, sasa swali ni hili ni kitu gani kilitengeneza hiyo automatic process ndani ya tumbo la mama hadi mtoto akapatikana, pili je, wazazi na viumbe hai vyote vinavyizaliana vilikuja kwa bahati tu au kuna kitu kilivileta hapa duniani??.

Majibu ya maswali hayo yanampeleka mtu MWENYE AKILI moja kwamoja kwa "Conscious minded being" causa causan ambaye ni Mungu.
 
Nguvu ya mafanikio ni nguvu zako mwenyewe na kuweka aibu pembeni.........wengi tunashindwa kutekeleza zile kazi zinazoweza kutupa mafanikio kwa sababu ya kuona aibu;mfano kuuza karanga kwa kutembeza,kuzibua vyoo n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…