Unawezaje kujua kuku kama amegongwa na nyoka baada ya kumchinja?
Wakuu leo asubuhi bandani kwa kuku nilisikia kuku wakirukaruka, kelele kama wanapigana na vurugu, baada ya kufungua Banda nimemkuta kuku mmoja akiwa taabani,ikabidi nimuwahi kisu kabla hajakata Moto.
Sasa sijajua ni nini kimempata.
Nahofia isije kuwa amegongwa na nyoka labda na kama ni nyoka jee nitaweza ona dalili zozote?
Ni kuku wa kienyeji, naomba kwa anayejua dalili za kuku aliyegongwa na nyoka anijulishe.
Mkuu ,huu uzi umepandishwa hapa Jumatano iliyopita lakini naona bado wanajamvi wanaelekea kutoa majibu.
Labda mm nichangie hivi:
1. Eneo unapofugia kuku wako , mazingira yaliyopo ni Rafiki kwa nyoka ?.i.e. kuna vichaka, msongamano wa vitu(makorokoro kibao) na kama uliwahi kuona nyoka eneo hilo.
2. Ulisikia nini kwanza/kabla kuku wako wakiwa katika kundi lao? Kama walikurupuka ghafla(Panic) na kukimbia huku na huko lakini wakielekeza vichwa vyao na kuangalia kwa mshangao sehemu moja ya banda(kama wanafugiwa ndani)?
3. Usimchinje huyo kuku-mfu bali mnyonyoe manyoya yake kwa uangalifu halafu anza kuangalia kwa uangalifu sehemu za kichwa: ukiona kuna vitobo au vimkwaruzo viwili hata kama vimeshajifunga/ziba anza kuhisi kagongwa na nyoka.
Chunguza kwa makini eneo la nyuma chini ya tundu la haja/kutokea yai na mapaja au mgongoni kati ya mabawa:Ukikuta /ona kuna vitobo/vimkwaruzo viwili hata kama vimejiziba hisi ni nyoka kagonga.
4.Ulipompasua huyo kibudu (huyo kuku-mfu) damu ilikuwa imeganda maeneo yaliyokuwa na vitobo(tuvidonda /mikwaruzo) na eneo linaonekana kuvimba japo kidogo?
5. Shika-shika maini au yapapase maini kwa kuyaminya kidogo(Hapa panahitaji utaalam na uzoefu): Je, yanamomonyoka au kusambaratika kirahisi? Tena angalia figo: Je, zimevia damu i.e. damu inaonekana kuganda ndani? Kagua moyo; Je, Mishipa ya damu hususan mshipa mkubwa
aorta) inaonekana kuganda damu? Tena angalia Mapafu; Je, yamevimba na kuweka damu au povu? Kama kuna damu au povu kwenye mapafu unaweza kuhisi nyoka.
6. Chunguza kama hakuna yai liliziba/pasukia ndani ya tumbo(Hii kitu husababisha kifo cha ghafla na kuku hudondoka chini na kutapatapa katika kufa kwake - (
egg bound peritonitis) na hivyo kupelekea mcharuka kwa kuku wengine.
Ukijiridhisha na yote hayo unaweza kusema ni nyoka au siyo nyoka.
NB: Sumu ya nyoka
HAIUI mara mbili. Narudia tena
HAIUI mara mbili i.e. Ikisha react katika mwili mmoja basi haipo tena hiyo ni
irreversible chemical change.
Nakushauri katika tukio kama hilo, Mtafute/Tafuta mtaalam wa mifugo wa Ugani aliye katika eneo lako. - Kwa nini upate shida ya uchunguzi wote huo nilioandika hapo juu wakati mwenye kazi hiyo yupo?
Hoja ya kula au kuto kula ni uamuzi wako.
Karibu tujuzane maarifa mkuu Asante.