Unawezaje kula chakula ulichopika mwenyewe?

Unawezaje kula chakula ulichopika mwenyewe?

maji ya gundu

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
3,070
Reaction score
4,698
Mungu ni mwema kwa wote.

Najiuliza unawezaje kula chakula ulichopika mwenyewe maana mi chakula nikipika kwa mikono yangu siwezi kukila yaani kinanikinai mapema.

Nyie kwenu vipi mnatumia mbinu gani kula chakula ulichopika mwenyewe.
 
Mimi inategemea na chakula Kama pilau au chapati ndio zinanishinda kula nikipka mwenyewe mpaka nijizungushe zungushe ndo nitaweza kula Kama wew ni kila chakula Basi ukimaliza kupka usile hapo hapo kaoge au fanya shughuli nyingne ukae mda kidogo ndo uje ule
 
Mimi inategemea na chakula Kama pilau au chapati ndo zinanishinda kula nikipka mwenyewe mpaka nijizungushe zungushe ndo ntaweza kula Kama wew ni kila chakula Basi ukimaliza kupka usile hapo hapo kaoge au fanya shughuli nyingne ukae mda kidogo ndo uje ule
Angalau wewe, me kitu chochote nikiweka mkono wangu tu siezi kula adi nimeshajulikana kwa mama ntilie ote, afu mazaga ya kupika yapo tu
 
Jichunguze,

Itakuwa wewe mwenyewe mapishi yako huyafurahii, huandai kwa usafi na ustadi na unadhifu, hauna ubunifu kila siku kifo cha mende.

Atiii..... umesema chakula gani?

Hujajua utamu wa selfie wewe.😋
 
Mimi inategemea na chakula Kama pilau au chapati ndo zinanishinda kula nikipka mwenyewe mpaka nijizungushe zungushe ndo ntaweza kula Kama wew ni kila chakula Basi ukimaliza kupka usile hapo hapo kaoge au fanya shughuli nyingne ukae mda kidogo ndo uje ule
Hatutofautiani kabisa, me nikipika wengine watakula me ntajipa shughuli hadi baada ya masaa labda mawili ndio nitaweza kula na kuenjoy chakula, njaa ikishanishika vizuri
 
Kwa kweli Mimi chakula Cha kupika mwenyewe ladha yake huwa siisikii
 
Mie sina hii kitu nikipika ugali wangu na samaki za kukaanga au dagaa na bamia. Naukamata sawa sawa.

Mungu ni mwema kwa wote

Najiuliza unaezaje kula chakula ulichopika mwenyewe maana mi chakula nikipika kwa mikono yangu siezi kukila yaani kinanikinai mapema

Nyie kwenu vp mnatumia mbinu gani kula chakula ulichopika mwenyewe
 
Mie sina hii kitu nikipiga ugali wangu na samaki za kukaanga au dagaa na bamia. Naukamata sawa sawa.
Daaaah asee mnaenjoy sana me labda nile kwa sapoti ya wengine ila peke angu kabisa siwezi mzee hili naliona kabisa tatizo
 
Kuna msemo hivi mpishi anashiba jikoni kwa kusikia harufu ya chakula itakuwa kwako ipo hivyo .
Mie kuna vyakula huwa nashiba hapo wakati napika nakua sina hamu kivile ila vingine nakula kweli.
 
Mungu ni mwema kwa wote

Najiuliza unaezaje kula chakula ulichopika mwenyewe maana mi chakula nikipika kwa mikono yangu siezi kukila yaani kinanikinai mapema

Nyie kwenu vp mnatumia mbinu gani kula chakula ulichopika mwenyewe
Haupiki unachotaka kula mkuu.
 
Haupiki unachotaka kula mkuu.
Hapana mkuu naeza nkapika chakula nnachotaka kula, nikishamaliza tu kupika hamu ya kula inakata, najipa moyo ngoja nikatembee kidogo ili hamu ikija nirudi kula ila final naangukia mgahawan nakula chakula kama nilichokiacha ghetto
 
Njaa haijakukamata au tusikuvungie sana haujui kupika.. fanya fanya ujifunze kupika ukionja unaonja bakuli zima..😂
 
Mungu ni mwema kwa wote.

Najiuliza unawezaje kula chakula ulichopika mwenyewe maana mi chakula nikipika kwa mikono yangu siwezi kukila yaani kinanikinai mapema.

Nyie kwenu vipi mnatumia mbinu gani kula chakula ulichopika mwenyewe.
Tunaopika mara kwa mara tusemeje.,au huwa unapenda kuonja sana jikoni?.

ila inategemea na siku
Kuna siku i love my own food hatariii...
Na siku zingine ukimaliza kupika basi hamu ya kula imeisha
 
Kiukweli naona mimi niko tofauti...Yaani chakula cha kupika mwenyewe ndio huwa nakifurahia saana..Nikiona mtu mwingine anapika huwa nawaza sijui kitakuwa kitamu kama ninachopika mimi..
 
Nashukuru Mungu hata nipike nn Bado ntakupa vzr tu yan sana
 
Back
Top Bottom