Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Nimekuwa nikifuatilia sakata la kuondolewa wamachinga katikati ya miji ili kuwapeleka maeneo maalum pembezoni ya mji. Ni hadithi inayonifanya kucheka sana kila nikiisikia. Kwanza ni jambo lisilowezekana kwa 90% na pili ni hadithi inayojirudia mara kwa mara. Serikali inaweza kuwaondoa wamachinga kinguvu (kwa muda fulani tu) kutoka katikati ya mji lakini haitaweza kuwapeleka kukaa na kudumu kwenye hayo maeneo mapya mbali na katikati ya mji.
Sababu za msingi za jambo hilo kutokuwezekana ni hizi.
1. Asili ya biashara ya umachinga ni kutangatanga, kufuata mikusanyiko ya watu, kudandia wateja barabarani na kusongamana. Mmachinga ni kama kuku wa kienyeji, anaishi vizuri kwa kumuacha azurure mitaani.
2. Wamachinga hawana tatizo na maeneo wanayofanyia biashara sasa, haya maeneo ya barabarani, holela holela na yasiyo rasmi wamachinga ndio wanayataka na wanayapenda sana.