Afrika ni shit hole countries!
Watu wakiambiwa wajadili faida za muungano Badala ya kujadili mambo ya uchumi wanajadili madaraka mpaka Bunge linavunjika. Wengine wanajadili Dini, ooh, hapa hatuitaki KUONA kanisa likijengwa mana kabla ya muungano hapakua na makanisa Mengi Sasa wanaimba mpaka Maeneo ya kujenga makanisa. Wengine nao Zanzibar IKIWA na uhuru kamili ugaidi utaongezeka na makanisa yatachomwa Moto.
Yaani watu wanajadili na kujenga Chuki tu juu ya Muungano Badala ya kujadili mambo ya uchumi namna Bora ya kutumia Muungano kukuza uchumi Wa nchi.
Leo hii Wazanzibari wanaona adui Yao ni Wakristo kuongezeka Zanzibar na wameaminishwa HIVYO na Wanasiasa wapumbavu.
CCM inatumia ujanja huo kupora uchaguzi na kuendelea kuwadidimiza Wazanzibari kiuchumi.
Adui Mkubwa Wa Wazanzibari ni CCM na serikali yake.
Sheria mbovu za Kodi na kiuchumi zinaiangamiza Tanzania ikiwemo Zanzibar.
Taifa linategemea Kodi za dhuluma na za kinyonyaji Kupitia bidhaa za kutoka Nje zinazotozwa Kodi KUBWA mara mbili ya Bei ya mtengenezaji Mwenyewe. Tanzania Bara wanapandisha Bei ya MAFUTA ya petroli, Redio,tv, magari , freji,Baiskeli,Bajaji,pikipiki, n.k. mara tatu mpaka nne ukilinganisha na Bei halisi ya bidhaa hiyo utafikiri bidhaa hizi Zina mbadala zinazozalishwa nchini.
Tulitegemea wapandishe Bei ya bidhaa Kama sukari,sementi, matakataka ya kutengenezea majuisi ya viwandani , Ngano, mahindi, Mchele, maharage, mafuta ya chakula Ili viwanda vya NDANI vizalishe Kwa wingi .
Bandari ya Zanzibar ilitakiwa iwe bandari huru kwenye Ukanda huu Wa Afrika Mashariki. Ili Nchi zote zije Tanzania Kununua bidhaa Badala ya kwenda Dubai,china n.k. Uchumi Wa Tanzania ungeimarika sana kutokana na Wageni na misururu ya wafanyabiashara Kuja Kununua bidhaa na kuzisafirisha kupitia bandari ya Dar es salaam Kwa malipo ya bandari tu na SIO Kodi. Kodi ingekua ni moja tu inayotozwa Tanzania Revenue Authority basi na ingekua inafanyikia Zanzibar. Zanzibar nao wangenufaika na udhuru Wa Bandari Tuu SIO kutoza Kodi. Ili kuepuka Kodi mara mbili kwenye nchi maja. Nchi ingekua na pato KUBWA sana ukilinganisha na huu ujinga na unyonyaji unaofanywa Kwa Watanzania kupitia TRA Na bandari ya DSM kuwaumiza watanzania akwa Kodi KUBWA mpaka watu wanapandisha Bei bidha ambazo nchi nyingine zote Duniani zipo chini isipokua Tanzania tu Kwa sababu ya Saisa za Kujaribu kuzuia uchumi Wa Zanzibar usiwe na manufaa Kwa Watanganyika na Wazanzibari wasinufaike na soko KUBWA la Ukanda Wa Afrika Mashariki.
Roho Mbaya za Mashati ya kijani yenye picha ya Mwenge ,Jembe na Nyundo ni ishara Mbaya ya kuwaponda watu kichwa Kwa kutumia Nyundo na kuwachoma moto Kwa kutumia Mwenge na Kisha kutumia Jembe kuchumba shimo la kuwazika WANANCHI hasa wanyonge.