Unayo akiba ya Tsh 150,000 kila mwezi na hutaki kufa Masikini, Kataa Ubinafsi, Soma Hapa

Be careful guys and warned.


Kuna jamaa ninamfaham humu jamii forum in personal kabisa huwa anakuja na hivi vimawazo vya kujikwamua mwisho wa siku ni utapeli.


Nasema tena kuweni makini.

Atakuwa Kevin Isaya Huyo.....Mimi kanitapeli aiseee
 
Be careful guys and warned.


Kuna jamaa ninamfaham humu jamii forum in personal kabisa huwa anakuja na hivi vimawazo vya kujikwamua mwisho wa siku ni utapeli.
Asante sana kwa taarifa

Nasema tena kuweni makini.

Asante sana kwa taarifa.
 
Mkuu mimi sina uzoefu Mkubwa kwenye biashara wala sijazaliwa familia ya kibiashara ila ni namna tu kujikwamua ndio tunatafuta. Kuhusu bidhaa labda nikupe mfano kuna Manufacturer nimeongea naye kuhusu KALAMU ZA BALAJ Zinazouzwa Tsh 100 kwa bei ya Jumla na Tsh 200 rejareja akasema atatoa kwa Tsh 44.4 per pen. Ila MOQ yake ni 2O" FCL.

- Sasa imagine hata kama kwa kalamu 1, ukilipa ushuru na gharama za matumizi yote ikawa Tsh 30, Jumla itakuwa Tsh 70/pen!
- So ukipata faida ya Tsh 30 kwa kuuza kwenye maduka ya rejareja kwa Tsh 100, kwa kalamu 200,000 utapata faida ya Tsh 6,000,000 na huo unaweza kuwa ni mzunguko au usambazaji wa Wiki au Wiki 2 tu !
 
Siwezi kumwamini mbongo.. Nimeapa.
Majuzi tu nimegombana na mtu ninayemwamini zaidi ya ndugu na bado bifu liko hot ile mbaya.
Just imagine, staff mate, college mate, tunashea everything, tuko level moja ya maisha, mshahara etc. Tuliaminiana kila kitu
Few months ago alinipa wazo la biashara nzuri kabisa, ambayo kila wiki inarudisha 10% ya hela uliyoweka. Na alinipa details zote za biashara husika. Akaniambia yeye ameweka 1m, na kila wiki anakula faida 100k. Baada ya kunishawishi sana nikachomoa laki 5. kwa majaribio. Wiki ya kwanza alisema nisubiri biashara ichanganye nichukue riba wiki ijayo.
Kweli wiki iliyofuata alinipa 50k. Baada ya hapo akawa anavusha wiki moja ananiambia oooh, mzigo umesumbua wiki hii mzigo umeadimika. Ikawa badala ya kupata laki 2 kwa mwezi nikawa napata laki 1. Baada ya mwezi wa kwanza kupita nikapata 50k baada ya wiki tatu, na sasa ni wiki 3 zingine sijapata hela, sababu nyingiiii. Nimemlazimisha arudishe mtaji sasa inaelekea mwezi kila siku chenga, nafikiria nikamfanyie fitna ambayo hatakuja kusahau.
Nimenyoosha mkono juu kwa wabongo. Bora Trump aje aniibie lakini siyo hapa
 
Pesa ni shetani mmoja mbaya sana nashangaa kwanini vuongozi wa imani hawamkemei.
 
Pole Sana
 

Mkuu? Pesa zitawekwa kwenye account ya kikundi? Na je watu wote 50 watakua Ndio signatories?
 
Wtz tuna mawazo mgando sanaa. Napitia Comment za watu ziko very negative sanaa.

Kwa nn tunakua wachoyo kiasi hicho umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Hata wadhamini, wafadhili na mabenki wanaamini zaidi vikundi kuliko Individual.
Ukitaka kufika mbali nenda na wenzakoo...
 
Mkuu wewe si ushasema unanifahamu ??
Hakuna sehemu nimesema nakufahamu, lete ushahidi acha porojo.


Nilisema kuna mtu namfahamu in personal huwa anakuja na project kama hizi mwisho wa siku ni utapeli. Kama anasoma hapa anajijua. Sasa naona unanibadirishia gia angani kuwa nimesema nakufahamu. Si kweli.


Njoo na taarifa zako muhimu kuanzia jina lako halisi ikiwezekana hii account omba kwa mods ifanyiwe editing uweke jina halisi. Tuambie unaishi wapi n.k ili watu wajilidhishe. Watu wameshapigwa hela zao unapaswa kuwa very unique kuwaondoa kwanza mawazo ya kutapeliwa kabla ya kufanya ushawishi wa project yako. Tusifanye vitu kwa kutafuta sympathy na mifano ya nchi za nje isiyoendana na mazingira ya kiafrika au kitanzania.


Mwisho, kwa maoni yangu idadi hiyo ni kubwa kwa biashara inayoanza. Najua utakuja na mifano yako ya kampuni za wachina au wazungu. Ila kwa mazingira halisi ya vijana na changamoto za kitanzania hiyo idadi ni kubwa sana. Tafuta vijana wasiozidi kumi wenye kujuana na kuaminiana mtekeleze hilo wazo with an option kuja kuongeza wadau huko mbeleni biashara ikikua.
 
Una mawazo mazuri sana,watanzania ni watu wa kuponda zaidi(I stand to be corrected).Ila nachoweza kwambia ni usilikatie tamaa jambo lako,tafuta watu wa karibu kama uliosoma nao,majirani,n.k!!!
" They will always ignore your Hustle but they will never ignore you when you get rich"

Stick to your Guns
 
Mkuu Daud1990 kwanza unakosea unaposema eti PROJECT YANGU ??!!

Hivi mtu anapokuja na wazo la kufungua duka la LAKI 3, akawa hana akakutafuta na wewe mkachanga kwa pamoja MKAANZISHA Kisheria ( Co-founding ) PROJECT inakuwa ni yake ???


Anyway pili mimi sijaweka namba ya simu mtu anitumie hela yake wala Akaunti yangu, wala sijamwambia mtu anipe hela yake.

Na tatu hili ni JAMBO LA HIARI tu Boss, wala hata lisikunyime usingizi sana !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…