Unayo ndoa lakini unatoka nje: justification

Waheshimu watoto wako!...mungu atkulipa mema zaidi.
 
Ameshawahi kwenda kwa daktari? Ameshajaribu dawa kama Viagra???

anatumia dawa za hospitali za kushusha sukari kwenye damu. sina uhakika kama ameshawahi kunywa viagra, ila najua anakunywa dawa za kisukari. kama alishakunywa basi nachojua ni kua haikufanya kazi
 
Sasa kumbe umeshaamua unataka kutoka...maswali ya nini?Hapa hutopata huo uhalalisho unaohitaji...kama unataka kuonyesha dhahiri kiapo chako ulichoapa siku ya ndoa kilikua cha uongo go ahead and do it kama nafsi yako inakuruhusu!

sijaamua lolote bado, nimejitoa hapa ili nisikie changamoto kutoka kwa wana JF, kwani naamini kuwa ukijua hili mwingine anajua lile, is just a matter of discussion and learning from others!
 
katika hili kweli FUTOTA umedhamiria: anaway, nasikia siku hizi kuna ndoa za aina tatu, 1. kupendana katika shida na raha, 2. kupendana katika shida tu, 3. kupendana nyakati za raha tu! inawezekana FUTOTA weye ulifunga hiyo aina ya tatu-kama kweli basi chomoka nje!:smash:
 

kupenda tunapendana, na hili tatizo halijaingilia kwa aina yoyote the love i have for my hubby, ila hii inahusiana moja kwa mojana mambo ya "lust". nasikia kwenye dini ya kiisilamu kama mke hapati tendo la ndoa kwa kipindi cha miezi 3 ni ruhusu kuomba talaka yake na ikatolewa bila kipingamizi. sasa inabidi kina baba watuelimishe tufanye nini (akina mama) inapotokea hali kama hii---"majogoo yanapoacha kuwika" kina baba wana jf tufahamisheni wajameni!
 

hiyo nyekundu! je ni wamama wangapi pia wanakosa uwezo kama huo-sijui yao inaitwaje??? lakini katika hili wababa tunanyanyapaliwa kwelkwel! usitafute kumuumiza mwenzio! hachana na fikra za kishetani hizo! ulikubali ukristo wapaswa kufwata uliyoyakiri kwa kinywa chako!
 

maumbile yanaruhusu akina mama ma "frigid" waendelee kuchapa kibarua cha kumridhisha mzee. wapo wanawake wengi hawajui nini raha ya tendo la ndoa, ufahamu wao ni kumstarehesha bwana na kuzaa watoto. mimi nimeamua kutoa hii topic hapa JF kwa sababu mara nyingi hapa tunasoma topics za kuonyesha egos za kina baba ....mara nyumba ndogo, mara house girl ananitaka, mara nifanye nini mtoto wa jirani anapenda etc etc, ujumbe mzima ukiwa ni kwamba wanaume wote (100%) are sexually fit, kitu ambacho si kweli. kuna tatizo kubwa sana la majogoo kutowika (erectile dysfunctions) katika jamii zetu, na wanaume wengi above 46 yrs si haba wanakumbwa na tatizo la poor sexual performance (mfadhaiko). nia nzima ya hii thread ni kuelimishana matatizo kama haya yakitokea katika ndoa mama afanyeje?
 

hapa ushauri ni huu: Imesemwa usizini, basi!!!!! Hakuna mjadala, hairuhusiwi kuzini, ukifanya na ulaaniwe mwombe mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…