Mlimazunzu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2010
- 415
- 53
Duu Umenikumbusha mbali sana. Hata kampuni ya Posta walikuwa wanatudangaya - wanatuuzia airform (karatasi ya kuandikia barua ambayo ni bahasha hiyohiyo) halafu imeandikwa " ukiweka kitu chochote ndani, haitasafirishwa kwa ndege" sasa sijui vijijini ndege zilikuwa zinatua wapi?
Halafu kwenye barua unaandika ' salaam zikufikie hapo ulipo, ama baada ya salaam je u hali gani? Upendapo kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya njema hofu na mashaka ni kwako uliye mbali na upeo wa macho yangu! haa haa haa du.
Ha ha ha ha yaani nimekumbuka kweli YCS nilikuwa nakwenda kutafuta wanawake tu wala si kusali ujana mbaya jamani. Barua unazimwaga kwa sana ila zilikuwa raha eti unarudi chumbani na barua ulizojibiwa unazirudia kuzisoma mara mbili mbili raha kweli enzi hizo