Unazungumzia CCM ipi?

Ukiona wazee wa chama wanatoka hadharani kujisifu juu ya yaliyomtokea mtangulizi,

Jua kuwa wameshagawana fito za nyumba Yao.
Lakini la kushangaza ni kwamba, pamoja na kugawana fito hizo bado wanaendelea kujenga nyumba ile ile waliyomo; iwe mbovu au imara, hayo hayawahusu wao, mradi manufaa yanawafikia wao.
 
[emoji119][emoji119]
 
Hapana.
Nilijua hunielewi ninaandika nini na inawezekana ukawa hunielewi kwa haya niliyoandika hapa.

Tuliyoshindwa kuelewana kati yetu huko nyuma yako wazi kabisa. Usidhani nimebadili msimamo juu yake. sasa.

Ni kwamba sikuelewi kwakuwa unaandika mambo magumu sana, au huna tabia ya kueleweka?
 
Ni kwamba sikuelewi kwakuwa unaandika mambo magumu sana, au huna tabia ya kueleweka?
Inawezekana yote kwa pamoja, au ikawa ni sababu ulizonazo wewe kutotaka kunielewa.
 
Bandiko linaeleweka. Dirisha la kuitikisa CCM baada ya kuondoka kwa Magufuli lilikuwa mwaka 2021 na kidogo 2022. Kwa kuruhusu wajipange upya na kurudi kwenye "comfortability" waliyofikia sasa, ni ngumu tena wale pro-Magufuli ndani ya CCM kuleta madhara ya kisiasa.

Hawa pro-Magu wataendelea kuchokonelewa na kutekenywa mara kwa mara ili kuangalia kama bado kuna masalia yaliyobaki yanayoweza kuibuka wakati usiotegemewa ila mtazamo wa CHADEMA kuhusu Magufuli na siasa zake unaipa CCM nafasi nzuri zaidi ya kupambana nao hao pro-Magu.

Kwa kumalizia ACT pia ni chama kitakachokuja kuisaidia sana CCM na naamini kilianzishwa kimkakati. Wakati CCM imeamua kukumbatia siasa za kibepari, ACT itatumika kama waendelezaji na watetezi wa sera za kijamaa zinazoachwa na CCM. Hii inafunga nafasi na uwezekano wa mtu mwingine kuja kuzitumia sera hizo kuiumiza CCM katika uwanja wa siasa.
 
CCMM ni DINI kama dini zingine,

Pia ni Kinyonga wa KIJANI na Manjano.

Tunakoelekea itatekwa na Aliye juu na itajipa umbo la Dini na kuja kuanzisha system yake ya kipekee duniani.

Mungu ataweka madhabahu yake hapa na tutakuwa msaada wa mataifa mengi.

Tusubiri.
 
"Mwaka 2021 na 2022", hii ilikuwa ni miaka ya "Kazi Iendelee". Kesi za akina Mbowe zikipamba moto huku zikichagizwa kwamba "washiriki wenzake tayari walishafikishwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo".

Hapana, hiyo miaka miwili haikuwa wakati ambapo pangeibuka upinzani ndani ya CCM, kwa sababu dereva mkuu alikuwa bado akitafuta njia ya kusawazisha na kuzima hilo kundi la upande wa Magufuli.
Hawa tayari wamekwisha dhibitiwa, ndani ya chama hakuna tena mwenye kufurukuta. Kumbuka, hoja ya mada ni kuwa, lengo kuu la haya makundi mbalimbali yaliyomo ndani ya CCM ni kufaidika wao, na siyo lazima kufaidika kwa taifa kwanza.
Kwa maana hiyo ni kwamba, masalia ya Magufuli yatakayokuwemo ndani ya CCM, sasa ni wakati wao kula kimya kimya ndani ya chama, siyo kula kwa kupiga kelele nyingi. Kundi la Samia ndani ya CCM chini ya Magufuli, ulisikia wakipiga kelele yoyote ile huku wakifaidika chini ya Magufuli?

Huo ndio muundo wa CCM ulivyo sasa hivi.

ACT Wazalendo? Ndani ya CCM? Sioni wanavyoweza kujipambanua. Sana sana hawa ni wa kumezwa tu na kuridhika na watakachotupiwa wakitafune.
 
Acha longolongo wewe mwarobaini wa kuiondoa CCM ni katiba mpya.
 
Usijidanganye alichotengeneza mwanadamu ni rahisi kukiharibu.
 
Tusubiri Hilo mpaka lini?
 
Andiko lako lingekamilika kama lingeonyesha mchango wa dola katika kuendelea kuiweka CCM mamlakani, CCM ni chama dola kuondolewa kwake kunahitaji mabadiliko makubwa katoka dola zaidi ya ubora wa chama pinzani tu.
 
Andiko lako lingekamilika kama lingeonyesha mchango wa dola katika kuendelea kuiweka CCM mamlakani, CCM ni chama dola kuondolewa kwake kunahitaji mabadiliko makubwa katoka dola zaidi ya ubora wa chama pinzani tu.
Hili ni wazo mkuu 'Yoda', sasa najaribu kuwaza,.... Hii "Dola" kwani ni nani? Inayo tofauti yoyote na CCM?
Viongozi wote walioko huko, wanapomaliza kazi zao huko, au hata kabla huwa hawashiki nyadhifa mbalimbali serikalini na hata ndani ya chama?

Sasa jaribu kuunganisha uhusiano huo na hoja ninayoitetea kwenye mada hii kuhusu CCM kuwa muunganiko wa makundi yenye maslahi tofauti tofauti, mengine yakiwa nje ya chama hicho, lakini yakiwa na washirika wao ndani ya chama chenyewe!

Kwa hiyo swali linabaki ni lile lile. CCM itaondolewaje madarakani wakati ikiwa na sura zote hizi zinazounganishwa na maslahi ya kila kundi ndani ya chama. Kila kundi kunufaika kwake ni uwepo wa CCM, hata hiyo "dola" unayoisema wewe. Nje ya CCM makundi haya hayana kitu, kwa hiyo uwepo wa CCM ndiyo nyenzo yao kuu, na hawawezi kamwe kuivuruga ndani kwa ndani.

Ndipo nilipoangukia kwa akina Sankara.

Lakini si lazima iwe hivyo. Inawezekana kabisa kukazuka chama ambacho viongozi wake ni maslahi ya nchi tu basi, wasioshawishika na haya ya kujinufaisha wenyewe kwanza. Hili linawezekana kabisa na ninaamini waTanzania wataunga mkono juhudi za viongozi hao.
Kama Magufuli, na mapungufu yote yale, kaweza kuwakoga nyoyo sehemu kubwa ya nchi, haiwezekani wenye dhamira ya mioyo ya kuwatumikia wananchi wasiungwe mkono.

"Dola" kupambana na wananchi waliodhamiria kuweka mabadiliko, tunajua ni nani huwa ni mshindi mara zote.
 
Akili kubwa sana,
 
Umesoma vzr na kumwelewa?, rudia tena kusoma ili uelewe halafu ndio uchangie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…