Unbeaten ya yanga: Ligi dhaifu ama timu imekuwa bora zaidi?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Kama kumbu kumbu zangu zipo sahihi,hii ni record ya Afrika inabebwa na yanga ama watachukua ya dunia kabisa.Hata ile yanga iliyocheza nusu fainali haikuweza kuweka record hii.

Kama ni ubora,basi ningetarajia klabu bingwa wangeweza kufika hata fainali.Hata hivyo wapo makundi shirikisho.Natarajia huko iwapo wao ni bora,wataongoza kundi lao na wanapaswa kufika fainali kabisa.

Kama hawatafanikiwa hivyo,basi lazima tujiulize hii unbeaten ni kwa vile yanga wanacheza ligi dhaifu?Ligi ambayo imedhaminiwa kwa pesa nyingi kuliko wakati wowote hapa nchini,inasikitisha sana kwamba ndiyo imekuwa ligi dhaifu kuliko zote ambazo zimewahi kutokea hapa nchini.Ligi hii hii dhaifu,kuna timu inacheza klabu bingwa Afrika na unaweza kushangazwa kwamba wakafanya vizuri sana.

Nawapongeza yanga kama ninavyokipongeza chama fulani ambacho huongoza kwa kura hata kwenye kituo alichopiga kura mgombea wa upinzani na familia yake yote unakuta mpinzani ana kura sifuri.
Nawapongeza kwa ushindi wa "kishindo"
 
Sasa umeweka hypothesis lakini umeiharibu kwa kukonclude kuwa hii ligi dhaifu.Hivyo hukuwa na sababu ya kujiuliza maswali.Inaweza kuwa Kuna udhaifu au uimara wa Yanga.Tunachopaswa kuangalia ni ubora wa mpira unaochezwa kwanza.
 
Ngada FC, Sembe FC, Pusha FC, wanasumbua sana.
 
Ngada fc mtakuja kuugua maradhi yasiyojulikana, kipindi simba anachukua ubingwa misimu 4 mfululizo uku marefa wakitoa masmuzi tata mengi ya kuibeba simba mbona ulikuwa umejificha kusikojulikana? Maswali aya ulitakiwa uyaulize kipindi kile kama ligi ilikuwa bora ama dhaifu sio sasa kwakuwa ubora wa yanga unajidhihirisha hadharani na utaonekana amnazo kuongea vitu vya ajabu mbele za wenye akili timamu
 
Labda niku ulize Simba inawezaje kufika robo fainali CAF harafu huku kwenye ligi inaboronga ina maana CAF ni dhaifu kuliko NBC PREMIER LEAGUE?
 
Sasa kipindi kile simba si ilifika mpaka robo fainali klabu bingwa?
Utata sasaivi upo kwasababu timu unbeaten imeshindwa hata kuvuka makundi klabu bingwa na huko shirikisho imepita kwenye tundu la sindano, tena dalili zinaonesha makundi itaenda kuchakazwa mbaya mbovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…