UNCHR : Wakimbizi 110,000 warejea Burundi toka Tanzania

UNCHR : Wakimbizi 110,000 warejea Burundi toka Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Rais Evariste Ndayishimiye apokea ujumbe wa UNHCR uliofika kumuona



Mwakilishi wa UNHCR Abdul Karim Ghoul ktk mazungumzo yake na Mh Rais Evariste Ndayishimiye amebainisha kuwa kutokana na utulivu Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi UNHCR wamefanikisha wakimbizi 110,000 kurejea Burundi.

Mwakilishi huyo wa UNHCR amempongeza Mh. Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi kuwezesha mazingira hayo ya utulivu. UNHCR UNHCR - The UN Refugee Agency yasema ingeweza kufanikisha kurejea kwa wakimbizi zaidi lakini janga la Covid-19 na changamoto zake zimezuia uwezekano wa idadi kubwa ya wakimbizi wa Burundi waliopo Tanzania kurejea kwa kufuata taratibu na viwango vya WHO shirika la Afya Duniani.

Burundi ina wakimbizi wengi Afrika ktk nchi za DR Congo, Namibia, Zambia, Afrika ya Kusini na huku Tanzania ikihifadhi wakimbizi wengi zaidi wa Burundi ktk makambi ya ukimbizi Tanzania.

Source : mashariki tv
 
Back
Top Bottom