UNCTAD Yatabiri Ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) la Tanzania Kufikia 5.8% Mwaka 2026

UNCTAD Yatabiri Ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) la Tanzania Kufikia 5.8% Mwaka 2026

Bwege2030

Member
Joined
May 10, 2025
Posts
97
Reaction score
197
UNCTAD Yatabiri Ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) la Tanzania Kufikia 5.8% Mwaka 2026 Huku Mfumuko wa Bei Ukishuka Hadi 2.8% Licha ya Kudorora kwa Uchumi wa Dunia.

Umoja wa Mataifa ya Hali ya Uchumi Duniani na Matarajio ya Mwaka 2026 (UNCTAD’s World Economic Situation and Prospects 2026) inatabiri kuwa ukuaji wa Pato la Taifa la Tanzania utakuwa 5.8% mwaka 2026 na 5.3% mwaka 2027 ukuaji huu unachochewa na mahitaji makubwa ya ndani, kuimarika kwa utulivu wa uchumi mkuu, mageuzi yanayoungwa mkono na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), uzalishaji mkubwa wa kilimo, na bei nzuri za dhahabu wakati huo huo, mfumuko wa bei unatarajiwa kushuka hadi 2.8%.


ni tofauti na mtazamo wa ukuaji wa uchumi wa dunia ambao unatarajiwa kuwa 2.7% pekee mwaka 2026 kutokana na migogoro ya kibiashara shinikizo la kifedha na uwekezaji mdogo.

Mtazamo wa Uchumi wa Dunia
UNCTAD inaeleza kuwa ingawa uchumi wa dunia umeonyesha ustahimilivu, mtazamo wa mbeleni umegubikwa na changamoto za kibiashara na kutokuwa na uhakika wa sera.
Ukuaji wa kimataifa unatarajiwa kushuka hadi 2.7% mwaka 2026 ikiwa ni kiwango cha chini kuliko mwaka 2025 na wastani wa kabla ya janga la Uviko-19 uliokuwa 3.2%.

Biashara ya kimataifa inatarajiwa kupungua kasi mwaka 2026 baada ya vichocheo vya muda mfupi kuisha na vikwazo vya kibiashara kuendelea.

Mfumuko wa bei wa dunia unatarajiwa kushuka kutoka 3.4% mwaka 2025 hadi 3.1% mwaka 2026, ingawa gharama kubwa za chakula, nishati, na nyumba bado zinaathiri kipato cha kaya zenye hali ya chini.

Mtazamo wa Uchumi wa Tanzania
Katika mazingira haya ya kidunia,Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi kubwa zilizoendelea kidogo (LDCs) zinazoonyesha utendaji mzuri wa kiuchumi.

Sababu kuu ni pamoja na:
Kuimarika kwa utulivu wa uchumi mkuu.
Mageuzi ya kiuchumi chini ya programu za IMF.
Uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo.
Bei nzuri za dhahabu katika soko la dunia.

UNCTAD inakadiria ukuaji wa GDP wa Tanzania kuwa 6.2% kwa mwaka 2025, kisha 5.8% (2026) na 5.3% (2027).

Mfumuko wa bei unakadiriwa kushuka kutoka 3.3% mwaka 2025 hadi 2.8% mwaka 2026, licha ya changamoto za mfumuko wa bei wa vyakula uliokuwa zaidi ya 10% kufikia Septemba 2025.


Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limeorodhesha mfuko wa pili wa ETF (Exchange Traded Fund) baada ya maombi ya ununuzi kuvuka lengo kwa 540% hata hivyo soko limepitia marekebisho ambapo benki za MBP na MKCB zimeshuka.

Mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi yaliongezeka na kufikia USD bilioni 17.5 kufikia Novemba 2025. Hii ilichochewa na mauzo ya dhahabu yaliyopanda kwa 42.1% (USD bilioni 4.7) na ongezeko la watalii waliofikia 2,315,478.
 
Back
Top Bottom